Meneja wa Programu za Vijana kutoka CSI Ester Mpanda(kushoto) akizungumza na mmoja wa mama aliyejifungua mtoto Njiti aliyefika katika zoezi la kutoa huduma za kiafya kwa watoto njiti iliyoandaliwa na Dorris Mollel Foundation na kufanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Programu za Vijana kutoka CSI, Ester Mpanda, timu ya Shirika la Childbirth Survival International(CSI) pamoja na timu ya Dorris Mollel Foundation wakiwafanyia usajili mama na mtoto waliofika kwa ajili ya watoto Njiti kufanyiwa uchunguzi na madaktari kutoka hospitali ya Muhimbili, Aga Khan na kuandaliwa na Dorris Mollel Foundation iliyofanyika Don Bosco jijini Dar es Salaam
Watoto Njiti wakisubilia kupewa huduma na Madakatari kutoka Muhimbili na Aga Khan wakati wa zoezi la kutoa huduma za kiafya kwa watoto njiti iliyoandaliwa na Dorris Mollel Foundation na kufanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.Madakatari kutoka hospitali mbalimbali za Jijini Dar es Salaam wakiendelea na kazi ya kuwachunguza watoto Njiti kwa ajili a kujua afya zao ili kuwaepusha na magonjwa mbalimbali yanayoweza kuwakabili wakati wa zoezi la kutoa huduma za kiafya kwa watoto njiti iliyoandaliwa na Dorris Mollel Foundation na kufanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Dorris Mollel Foundation, Dorris Mollel(wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Shirika la Childbirth Survival International(CSI) waliofika kwa ajili ya kutoa mchango kwa Dorris Mollel Foundation.
SHIRIKA la Childbirth Survival International(CSI) limesema linatoa pongezi na kuunga mkono jitihada ambazo zinafanywa na Taasisi ya Dorris Mollel ambayo imejikita kusaidia watoto njiti ikiwa pamoja na kuhakikisha wanapata malezi yanayostahili pamoja na kufuatilia malezi na makuzi yao.
Akizungumza wakati wa tukio lililoandaliwa na Dorris Mollel Foundation la kutoa huduma za afya kwa watoto njiti lililofanyika Don Bosco jijini Dar es Salaam, Meneja wa Programu za Vijana kutoka CSI Ester Mpanda amesema kwamba shirika lao linajihusisha na afya ya mama na mtoto hasa katika kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama na mtoto wakati wa kujifungua.
"Hivyo tuko hapa kwasababu ya kusadia kazi zinazofanya na Dorris Foundation kwani ni kitu ambacho sisi pia tunakifanya kwa njia moja au nyingine maana tumejikita katika kuhakikisha mama na mtoto wanakuwa salama.
"Hivyo tumefurahishwa na kazi yake na tunachokifanya CSI ni kumuunga mkono na kumtia nguvu kwa kazi anayofanya ili aweze kufikia jamii kubwa,"amesema Ester Mpanda.
Kuhusu ujumbe wa CSI kuelekea siku ya mtoto njiti Novemba 17, 2020, Ester Mpanda amesema wanaiomba jamii hasa inayoishi na mtoto Njiti kuhakikisha anafuatilia vema na kufuata ushauri wa madaktari kuhakikisha mtoto anakuwa salama na tukio lililoandaliwa na Dorris Foundation la kuandaa madaktari bingwa kwa ajili ya kuangalia maedeleo ya watoto njiti linatoa nafasi kwa wazazi kujua maendeleo ya watoto.
"Tukio hili ambalo limefanyika siku ya leo ni muhimu, jamii isipuuze kwani inatoa nafasi ya mzazi au mlezi kujua hali za watoto wao, kwani mtoto njiti maana yake amezaliwa kabla ya muda , hivyo afya mara nyingi inakuwa sio nzuri.
"Hivyo wanapokuja kujua hapa inakuwa rahisi kujua hali za watoto kama kuna viashiria vya ulemavu au wanaendelea vizuri, jamii inaposikia vitu vya aina hiyo waitikie mwito kwani vinafaida kwa mtoto na wazazi kwa ujumla,"amesema
Alipoulizwa kuhusu jitihadaza za CSI katika kusaidiana na Serikali na wadau wengine kupunguza vifo vya mama na mtoto, Mpanda amesema kwa sasa hivi hali ni nzuri na kwamba hata hotuba ya Rais John Magufuli imeeleza jinsi vifo vya mama na mtoto ambavyo vimepungua.
"Vifo vimepungua sana na kusababu nyingi ambazo zimesababisha, mbali ya elimu ambazo wadau tunatoa tukiwemo sisi CSI, lakini Serikali imefanya kazi kubwa kuboresha miundombinu, kuna zahanati, vituo vingi vya afya na hospitali.
CSI tunashirikiana na Serikali kwa mambo mengi tunayofanya na kwa hakika imefanikiwa kupunguza hivyo hivyo.Mkakati wetu i kuendelea kusehemu ya timu ya Serikali na kuhakikisha tunaendelea kutoa elimu ya uzazi salama kuanzia ngazi ya chini kwa makundi ya vijana mpaka kwa mama wajawazito na wazazazi kwa ujumla,"amesema.
Alipoulizwa nini ambacho CSI wanafanya katika kupunguza vifo vya mama na mtoto , Mpanda amesema wamekuwa wakitoa elimu ya uzazi salama , wamekuwa wakisaidia vifaa vya kuzalia , kutoa elimu kwa jamii kutambua viashiria vya hatarishi, wanazo programu maalum kwa ajili ya wasichana inayozungumzia masuala ya uzazi na viashiria hatari vya uzazi ambavyo wakiviona vile wanajua wanatakiwa kuanza kliniki mapema.
"Kwa hiyo tumekuwa tukitoa elimu kwa ujumla kuhusu masuala ya uzazi na hasa uzazi salama kuanzia mimba ikiwa changa hadi pale inapofika miezi tisa na hiyo ndio imekuwa kazi ya CSI kwa muda mrefu ma mpaka sasa.
"Tumefika katika mikoa 10 nchini Tanzania na tunaendelea kufanya. Pia sio hapa tu bali tupo nchini Rwanda, Kenya, Somalia, Uganda na Marekani ambako ndiko kuna makao makuu yetu.Hivyo hata ukiangalia mitandao yetu ya kijamii ya Instagramu, facebook, utaona kazi ambazo CSI tunafanya,"amesema Mpanda.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake