Friday, December 11, 2020

SPIKA JOB NDUGAI AMUAPISHA UBUNGE PROF. MANYA JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge, Job Ndugai akimuapisha Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Prof. Shukrani Manya tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai 
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai (kulia) akimkabidhi vitendea kazi Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Prof. Shukrani Manya mara baada ya kuapishwa Ubunge na Spika wa Bunge, Job Ndugai (hayupo kwenye picha) tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Prof. Shukrani Manya akizungumza na watumishi wa ofisi ya Bunge na wageni waalikwa mara baada ya kuapishwa Ubunge tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai (wa pili kulia)
Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Prof. Shukrani Manya (wa pili kulia) tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai na Waziri wa Madini, Dotto Biteko

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments: