Sunday, December 6, 2020

VIVUTIO VYA TANZANIA KUTANGAZWA KWENYE TELEVISHENI YA UFARANSA

Mkuu wa Ofisi ya TTB Kanda ya Kaskazini Bi. Esta Solomoni akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro pamoja na Sebastian Verlet (katikati) na Maxime Souville Wataalam kutoka Bo Travail ya Ufaransa

Wataalam kutoka Bo Travail ya Ufaransa, Sebastian Verlet (kushoto) na Maxime Souville wakionyesha mifuko waliyokabidhiwa na TTB yenye vipeperushi vyenye taarifa za vivutio vya utalii vya Tanzania.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa imeandaa ziara ya Wataalmu nane watengeneza filamu za utalii kutoka katika kampuni ya Bo Travail ya nchini Ufaransa kwa lengo la kutengeneza filamu ya kitalii iliyopewa jina la “Tanzania Beautiful Escapes” pamoja na makala maalumu ya lugha ya kifarasa ambazo zitaonyeshwa kwenye Televisheni ya Ufaransa.

Akizungumza punde baada ya kundi la kwanza la wataalam wawili wa Bo Travail kuwasili katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro tarehe 5 Disemba, 2020, Mratibu wa safari hiyo ambaye ni Mkuu wa ofisi ya TTB Kanda ya Ziwa, Bi. Glory Munhambo alisema “TTB imefaya jitihada za makusudi kushirikiana na kampuni ya Bo Travail ambayo ni watengeneza filamu mashuhuri za utalii nchini Ufaransa kuja Tanzania kutayarisha filamu na makala kwa kutumia baadhi ya maeneo ya vivutio vya utalii vya jiji la Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Karatu kwenye vikundi vya utalii wa kiutamaduni na visiwa vya Zanzibar .

Bi. Glory aliendelea kusema kuwa “Wataalamu hawa watakuwa nchini kwa muda wa siku 14, ambapo wanawasili kwa makundi mawili tofauti, kundi la kwanza la watu wawili limeingia leo na kuondoka Disemba 18, 2020 na kundi la pili la wataalamu wanne litawasili nchini Disemba 8 mpaka Disemba 18, 2020, huu ni mwendelezo wa mpango mkakati wa TTB wa kutumia vipindi maalumu vya televisheni za nchi mbalimbali ili kuweza kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi katika masoko ya utalii na kuwavitia ili waje kuvitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania.”

Ufaransa ni moja ya masoko makuu ya utalii ya Tanzania barani ulaya ambapo kwa takwimu za mwaka 2019 zinazotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonyesha Tanzania ilipokea jumla ya watalii 56, 297 kutoka Ufaransa.

No comments: