Tuesday, January 5, 2021

RIDHIWANI KIKWETE AHANI MSIBA WA MTOTO WA NYERERE-MSASANI

MBUNGE Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amefika nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhani msiba kufuatia kifo cha Rosemary Nyerere aliyefariki dunia Januari Mosi mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Ridhiwani Kikwete pia ameweza kusaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa familia ya Nyerere ikiwemo watoto na wajukuu katika makazi ya Baba wa Taifa, Msasani Jijini Dar es Salaam.

Awali akitoa pole kwa mtoto wa Baba wa Taifa, Makongoro Nyerere, Ridhiwani Kikwete alieleza kuwa, familia ya Nyerere imepata pigo kubwa hivyo kuungana na familia.

“Tunaungana kwa pamoja katika msiba huu mzito hakika umetugusa sote. Kwa niaba ya familia yangu pamoja na Wanachalinze tunatoa salamu za pole kwa Wanafamilia ya Nyerere.” Alieleza Ridhiwani Kikwete.

Rosemary alikuwa miongoni mwa watoto saba wa Mwalimu Nyerere.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake