Thursday, January 14, 2021

TAARIFA YA MSIBA WA MZEE KAPANGA

 *TAARIFA YA MSIBA WA MZEE KAPANGA*

Ndugu wanajumuhiya,
kwa masikitiko makubwa, uongozi unawatangazia msiba mzazi wa kiongozi na mwanajumuiya mwenzetu ndugu Peter Kapanga ambaye amefiwa na baba yake mzazi mzee Alfred Semuwunge Kapanga , January 14th, mjini Dar-Es-Salaam,Tanzania. Ndugu Peter yupo safarini kuelekea Tanzania kwa ajili ya msiba huo mzito.

Kama ilivyo kawaida uongozi umepitia vigezo vikuu muhimu vya taratibu za misiba kama ifuatavyo:
*1. Mfiwa ni mwanajumuiya aliyejiandikisha kwenye jumuiya.*
*2. Mfiwa ni mwanajumuiya anayechangia misiba ya wanajumuiya wengine.*
*3. Mfiwa ni mkazi wa DFW zaidi ya miezi 6.*

Hivyo uongozi umeridhika na vigezo hivyo na kuidhinisha rasmi zoezi la rambirambi ya msiba huu ambao umetugusa sote. 
Kisha tuma spapshot ya cashApp kupitia group la jumuiya au viongozi. Tafadhali andika majina yako kamili kurahisisha utunzwaji wa kumbukumbu zote za rambirambi kupitia database ya jumuiya. 
Asanteni kwa ushirikiano wenu na Mungu awabariki kwa kujitoa kwenu.
Tafadhali wasilisha rambirambi zako moja kwa moja kwa mfiwa ndugu Peter Kapanga kupitia:
*Zelle/Ph: (214) 394-7906*
*CasApp: $PeterKapanga*

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake