Thursday, January 7, 2021

WAFUASI WA TRUMP WAANDAMANA, BUNGE LA MAREKANI LA KEMEA, TWITTER YAIFUNGIA AKAUNTI

 

Polisi wakiwazuia wafuasi wa Rais Trump nje ya jengo la Bunge linalojulikana US Capitol baada ya wa wafuasi hao kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais  kutokkana  na kile wanchodaid uchakachuaji wa matokeo hayo.
Wamoja ya Wabunge wakikimbia kutafuta sehemu salama kuokoa maisha yao baada ya baadhi ya wafuasi hao kuingia ndani ya jengo la Bunge.

Bunge la Marekani limelaani vikali waandamanaji wafuafi wa Rais Donald Trump kwa kufanya maandamano yaliyosababisha mtu mmoja kupoteza maisha.

Bunge la Marekani lililazimika kukatisha shughuli za mchana kutokana na wafuasi hao kufanya vurugu na wengine kulazimisha kuingia ndani ya Bunge kutokana na wafuasi hao kudai kushindwa kwa Rais Trump kulitokana na uchakachuaji kwa baadhi ya majimbo.

Baadae usiku Bunge liliendelea na hii ni baada ya vurugu za waandamanaji hao kutulizwa na polisi na huku wakiamriwa kutawanyika katika eneo hilo.

Wabunge waliowengi wa vyama vyote waliopata nafasi ya kujadili swala hilo walilaani vikali na wengi kutupiana lawama wenyewe na kusisitiza ni lazima kuwaambia wananchi ukweli kwamba Rais Mteule Joe Biden ameshinda kihalali na hakukua na uchakachuaji wowote. Na kama hiyo haitoshi, walielezea na kutolea mfano majimbo yaliyolalamikiwa na ikiwemo mahakama kutolea ufafanuzi kwamba swala la uchakachuaji wa matokeo haukuwepo.

Mtandao wa Twitter jana ulifunga akaunti ya Rais Trump kwa kilichoelezwa ya kuwa inachangia uchochezi kwa kutowaambia wafuasi wake ukweli, mitandao mingine ya kijamii iliyoshusha baadhi ya matangazo mengine ya Rais huyo ni pamoja na facebook

Maya wa Washingto, DC alitangaza hali ya hatari siku ya jana kuamkia leo Alhamisi Januari 7, hali ya hatari hiyo iliwataka watu wote wawe majumbani isipokua kuwa wale pekee wanaotoa huduma kwa jamii ndio watakao ruhusiwa kuwa barabarani.

No comments: