Monday, February 1, 2021

Ahmad Ahmad afutiwa adhabu

BAADA ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kusimamishwa na mahakama ya usuluhisho wa masuala ya soka (CAS) kwa miaka mitano kutokana na kilichodaiwa kuwa matumizi mabaya ya ofisi Novemba 23 mwaka jana, Rais huyo ameruhusiwa kuendelea na majukumu yake baada ya makama hiyo kijiridhisha na kukuta hana hatia.

Ijumaa iliyopita ya Januari 29 CAS walisitisha vikwazo vyote alivyokuwa amewekewa Ahmad na kamati ya maamuzi ya FIFA na kumruhusu kuendelea na majukumu yake kama Rais.

baaada ya kupata taarifa hiyo liyekuwa kaimu Rais wa CAF, Constant Omari ambaye pia ameonesha nia ya kugombea kiti hicho kwenye uchaguzi ujao, aliitisha kikao cha dharura kwa kamati ya utendaji ya CAF kupitia mtandao ambapo alieleza uamuzi huo wa CAS na kumkaribisha tena Ahmad Ahmad kuendelea na majukumu yao.

Kwa upande wa Ahmad amezishukuru mamlaka zote zilizofuatilia mchakato huo na leo Jumatatu atakutana na kamati ya utendaji ya CAF tayari kwa kuzungumza muendelezo wa kazi zake kama Rais.

Pia Ahmad Ahmad ametoa shukrani za dhati kwa Constant Omari kwa kukaimu vyema nafasi yakje na kusimamia, kuendeleza mikakati iliyokuwa imewekwa na Ahmad ndani ya kipindiu alichokuwa kwenye uangalizi.

Ikumbukwe Ahmad Ahmad alichaguliwa kuwa Rais wa CAF mwaka 2017 na alikutwa na hatia hiyo Novemba 3 mwaka jana.

MWANASPOTI

No comments: