Kipa wa Simba, Aishi Manula (mwenye kofia) akiwa amezungukwa na mashabiki kabla ya kutaka kuibiwa na kijana aliyepo upande wake wa kulia (fulana ya njano), hata ivyo kijana huyo alishindwa baada ya Manula kumshtukia na kumshika mkono wake ili asimwibie simu. Picha na Michael Matemanga
KIKOSI cha Simba kimewasili nchini mchana wa leo Februari 14 kikitokea Adis Ababa, Ethiopia na moja ya tukio lililoshtua kwenye mapokezi hayo ni shabiki mmoja alitaka kumuibia simu golikipa wa Simba, Aishi Manula.
Tukio hilo limetokea wakati wachezaji wa Simba wakiingia kwenye basi la timu hiyo kwa ajili ya kwenda kambini kwa mchezo ujao wa Ligi dhidi ya Biashara, mamia ya mashabiki ambao walijitokeza uwanjani hapo walikuwa wakiimba jina la mchezaji mmoja baada ya mwingine huku wengine wakipigana vikumbo kutaka kupiga nao picha 'selfie'.
Katika purukushani hizo, alionekana shabiki mmoja aliyejaribu kumuibia simu ya mkononi, Aishi Manula lakini kipa huyo alimshtukia kabla ya kutekeleza wizi huo na kumdaka mkono uliokuwa unachomoa taratibu.
Kipa huyo namba moja wa timu ya taifa la Tanzania 'Taifa Stars' baada ya kuhakikisha simu yake ipo salama aliachana na kibaka huyo kisha akaenda kupanda bus la timu moja kwa moja kwa safari ya kwenda kambini.
Kocha wa timu hiyo, Didier Gomes amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United Alhamisi Februari 18 kabla ya kuanza hesabu za namna ya kukabiliana na Al Ahly.
Vijana wa Gomes wamerejea kishujaa nchini kufuatia kuibuka kwao na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita huko Kinshasa, DR Congo.
Mara baada ya kutua nchini huku wakipokewa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo licha ya awali kutangazwa kuwa hakutakuwa na mapokezi kama ilivyozoeleka, Gomes aliyekuwa akishangiliwa na mashabiki hao, alisema nguvu zao wanazielekeza kwenye mchezo huo ambao watakuwa ugenini.
"Tunamchezo mgumu na muhimu mbele yetu ambao tutacheza alhamisi tukiwa ugenini. Tunapaswa kushinda huu mchezo kabla ya kuhamishia mawazo yetu kwa Al Ahly," alisema kocha huyo Mfaransa na kuongeza.
"Kuna mapungufu ambayo tunapaswa kuyafanyia kazi kama timu tukiwa mazoezini ili kuhakikisha tunakuwa bora zaidi," alisema Gomes.
Gomes alitumia nafasi hiyo, kuwapongeza wachezaji wake kwa kusema walicheza vizuri mchezo wao uliopita dhidi ya AS Vita,"Walionyesha ukomavu kwa kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu lakini bado safari ndio kwanza imeanza."
Wakati wachezaji wa Simba wakiingia kwenye basi la timu hiyo kwa ajili ya kwenda kambini kwa mchezo ujao wa Ligi dhidi ya Biashara, mamia ya mashabiki ambao walijitokeza uwanjani hapo walikuwa akiimba jina la mchezaji mmoja baada ya mwingine huku wengine wakipigana vikumbo kutaka kupiga nao picha 'selfie'.
Katika purukushani hizo, alionekana shabiki mmoja aliyejaribu kumuibia simu ya mkononi, Aishi Manula lakini kipa huyo alimshtukia kabla ya kutekeleza wizi huo na kumdaka mkono uliokuwa unachomoa taratibu.
Kipa huyo namba moja wa timu ya taifa la Tanzania 'Taifa Stars' baada ya kuhakikisha simu yake ipo salama aliachana na kibaka huyo kisha akaenda kupanda bus la timu moja kwa moja kwa safari ya kwenda kambini.
No comments:
Post a Comment