Mwenyekiti Kamati na Itifaki wa UWAMBESO Bw.Tumsifu Mwasamale,akiwatambulisha Waheshimiwa wabunge a Mikoa ya Mbeya na Songwe waliofika katika Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu wa UWAMBESO Bi.Baleke Moses,akisoma taarifa kuhusu Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe wakati wa uzinduzi wa umoja huo uliofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa UWAMBESO Mhe.Diwani Nsubi Bukuku,akizungumza kwenye uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akizungumza na wananchama wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Wanachma wa UWAMBESO wakifatilia hotuba ya Naibu Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya (CCM) Mhe.MaryPrisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji,akitoa neno wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwanachama Mpya wa UWAMBESO ambaye ni Mbunge wa Wazazi Taifa Mhe.Bahati Ndingo,akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa (CCM) Mkoani Songwe Mhe.Japhet Hasunga,akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Kikundi cha Ngoma ya Asili kutoka Mkoani Mbeya Kikiburudisha wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika es Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akicheza ngoma na Kikundi cha ngoma ya asili kutoka Mbeya wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akiwa na Waheshimiwa wabunge na Wanachama wakicheza ngoma za asili wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akiwa na wabunge pamoja na viongozi wa UWAMBESO wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akiwa na wabunge pamoja na viongozi wa UWAMBESO wakionyesha vitabu vyenye katiba ya Umoja huo mara baada ya kukata utepe wa kuashiria Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akikabidha Vyeti kwa Wanachama Waasisi wa UWAMBESO mara baada ya kuzindua Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akikabidhiwa cheti cha Pongezi na Mwenyekiti wa UWAMBESO Bw. Nsubi Bukuku,mara baada ya Naibu Spika kuzindua Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa UWAMBESO Bw.Nsubi Bukuku,akimkabidhi Cheti cha Pongezi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya (CCM) Mhe.MaryPrisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, mara baada ya Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa UWAMBESO Bw.Nsubi Bukuku,akimkabidhi Cheti cha Pongezi Mbunge wa Jimbo la Vwawa (CCM) Mkoani Songwe Mhe.Japhet Hasunga mara baada ya Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa UWAMBESO Bw.Nsubi Bukuku,akimkabidhi Cheti cha Pongezi Mwanachama Mpya wa UWAMBESO ambaye ni Mbunge wa Wazazi Taifa Mhe.Bahati Ndingo, mara baada ya Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akiwa na wabunge pamoja na viongozi wa UWAMBESO,akikata Keki kuashiria Harambee ya kuchangisha Fedha kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa UWAMBESO wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson,akiwa na wabunge pamoja na viongozi wa UWAMBESO katika picha za pamoja mara baada ya kuzindua Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe (UWAMBESO) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
NAIBU Spika Dk Tulia Ackson ametoa rai wa watu wa kutoka Mikoa ya Mbeya na Songwe kushiriki katika maendeleo ya mikoa yaoz Ikiwa ni pamoja na endeleza maeneo walikotoka.
Dk Tulia ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati akizindua Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe(UWAMBESO-Dadoka).
Dk.Tulia amesema suala la maendeleo ya mikoa ya Mbeya na Songwe ni Jambo muhimu ambalo Wana-UWAMBESO Dodoma wanapaswa kuzingatia.
“ Mambo yanayokea hapa makao makuu na kutawanyika nchi nzima ikiwemo mikoa ya Songwe na Mbeya, mkoa hapa kwenye maofisi mbalimbali na pengine mkishirikiana na sisi wabunge tunaweza kusumuma mambo ili sehemu zetu kule zipate maendeleo.” “
Tunataka maendeleo yafike kule, wale watu walivyotuchangu sisi kuja Dodoma ni ili tuje tuwasemee, lakini kusema ni jambo moja na kufanyika kule ulikotoka ni jambo la pili, na baadhi yenu hapa ni sehemu ya watu wanaoweza kusukuma haya mambo.
“ Kwa hiyo moja wapo natamani UWAMBESO Dodoma iwe inafanya ni kutuletea wabunge mawazo yenu kuhusu maendeleo ya kule nyumbani, tushauriane humu ndani tunaweza kuwa na wajenzi, wachora ramani.”
Pia Dk Tulia amewamizia wanaUwambeso kuhakikisha anaendeleza katika katika vijiji tulivyotoka kwa kujenga nyumba bora nyumbani na kuwataka kuwa mfano kupeleka maendeleo katika maeneo yao.
“ Tunaweza kujenga mjini na wakati wa kusindikizana ikawa mitihani, UWAMBESO tuwe sehemu ya kushauriana sio tukishasindikizana wakati wa kurudi ni mjadala wa kukosekana kwa choo, wewe peleka mjengo wako sasa tuachie wabunge tukusemee barabara ya kufika hapo, yale ya kutekelezwa na Serikali tuleteeni tutayasemea”
Aidha, Dk Tulia kuwapongeza kwa kuanishaumoja huo Wenye malengo yenye tija katika kukuza uchumi na wanachama na kuhimiza kuwa changamoto ndogo ndogo zisivvurugene Umoja na kuwataka kuzingatia katiba.
Dk Tulia pia alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha wanaongeza wigo wa wanachama kutoka katika Wilaya zote za mkoa wa Dodoma na si kwa Dodoma Mjini na baadaye kuangalia kufika mikoa mingine.
Awali Katibu wa UWAMBESO Dodoma, Baleke Mwakanosya amesema kuwa umoja huo unawanachama takribani 140 ikiwa na malengo ya kushirikiana kwenye raha na shida.
Bi.Mwakanosya amesema kuwa umoja huo unamikakati Mungu ya kuhakikisha unawainua wanachama kiuchumi kwa kuanzisha chama Cha kuweka na kukopa(saccos)
No comments:
Post a Comment