ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 13, 2021

RAIS MHE.SAMIA AMEOMBWA KUTENGENEZA UTARATIBU MZURI WA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA ARDHI

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameombwa kutengeneza mfumo na utaratibu mzuri wa kushughulika masuala ya umilikaji wa ardhi ,nyumba,mashamba na viwanja kwa wanadiaspora na Watanzania kwa ujumla.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Askofu mkuu wa Kanisa la GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY Dkt. Charles Gadi wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema suala la Wanadiaspora katika umiliki wa Ardhi hapa nchini linahitaji msaada wa Rais.

Aidha Askofu Gadi amemuomba Rais kulishauri Bunge kutumia mfumo wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar ili kuwezesha watanzania wanaoishi nje na wawekezaji wengine kuingia na kufanya biashara kwa urahisi hapa nchini .

Akizungumzia suala la biashara askofu huyo amesema kuna baadhi ya sheria na Taratibu ambazo zinadaiwa kutokuwa rafiki na kudai zinaikosesha Taifa mapato, huku akitaja moja wapo ni sheria ya kuiza malori yenye uzito na vipimo/viwango

Dkt. Gadi amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa maagizo ya kupunguza urasimu kwenye masuala ya ardhi hususan kwa wawekezaji pamoja na kupongeza kauli aliyoitoa wakati akiongea na wazee wa Dar es Salaam kwa kukubali kuteua watu wote wenye uwezo kwenye nafasi mbalimbali bila kujali vyama au itikadi zao.

 

No comments: