Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Kololo, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika uwanja huo uliopo Kampala nchini Uganda leo tarehe 12 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Marais wengine wa Nchi za Kiafrika pamoja na Wageni wengine waliohudhuria sherehe za Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika Uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni akikagua Gwaride la Jeshi la Uganda huku
akiwa kwenye Gari la wazi mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Uganda katika
kipindi cha muhula mwingine katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa
Kololo, Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni akizungumza mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment