Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Catherine Bamwenzaki akifungua Kikao cha Kamati ya Kitaalamu ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo ya Ikolojia (EBARR) kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt. Andrew Komba kilichofanyika leo Mei 10, 2021 jijini Dodoma.
Washiriki wakiwa katika Kikao cha Kamati ya Kitaalamu ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo ya Ikolojia (EBARR) kutoka Halmashauri za Wilaya za Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa (Dodoma), Mvomero (Morogoro), Simanjiro (Manyara, Wilaya ya Kaskazini A (Mkoa wa Kaskazini Unguja) kilichofanyika Mei 10, 2021 jijini Dodoma.
Meneja wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo ya Ikolojia (EBARR) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Nyarobi Makuru akifafanua jambo wakati wa Kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu wa mradi huo kilichofanyika leo Mei 10, 2021 jijini Dodoma.
Washiriki wakiwa katika Kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo ya Ikolojia (EBARR) kutoka Halmashauri za Wilaya za Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa (Dodoma), Mvomero (Morogoro), Simanjiro (Manyara, Wilaya ya Kaskazini A, (Mkoa wa Kaskazini Unguja) kilichofanyika leo Mei 10, 2021 jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kitaalamu ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) wametakiwa kupitia changamoto zote za utekelezaji wa mradi huo zilizojitokeza na kupendekeza hatua za kuchukua.
Wito huo umetolea leo Mei 10, 2021 na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba alipokuwa akifungua Kikao cha Kamati ya Kitaalamu ya mradi huo jijini Dodoma.
Dkt. Komba alisema kazi kubwa ya kikao hicho kupitia taarifa za utekelezaji wa mradi wa EBARR, matumizi ya fedha, mpango kazi na bajeti ya mradi kwa mwaka 2021 pamoja na kutoa mapendekezo kwa kamati ya uendeshaji wa mradi (Project Steering Committee – PSC) kwa ajili ya maamuzi.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo yameonekana katika sekta mbalimbali za uzalishaji nchini ikiwemo kilimo, mifugo, maji, nishati, maliasili, miundombinu na usafirishaji.
Alizitaja athari hizo kuwa ni ukame, mafuriko, maporomoko ya udongo, ongezeko la joto, kuibuka na mlipuko wa magonjwa ya mazao, mifugo na binadamu na uwepo wa viumbe vamizi na kuwa jamii maskini hasa za vijijini huathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.
“Katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, serikali kupitia ofisi ya makamu wa rais inaratibu utekelezaji wa mradi wa ebarr kwa kushirikiana na sekta nyingine za kilimo, mifogo, na maji na halmashauri za wilaya nne tanzania bara na wilaya moja zanzibar.
“Mradi unatekelezwa katika wilaya za Mvomero (Morogoro), Simanjiro (Manyara), Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa (Dodoma) na Kaskazini A, (Unguja). Maeneo ya mradi yalichaguliwa kwa kuzingatia maeneo yanye ukame yenye jamii za wakulima, wafugaji, na wavuvi,” alisema.
Aidha, Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa chini ya mradi wa – EBARR, Kamati ya Uendeshaji wa Mradi (PSC) hukutana kila mwaka kujadili na kupitisha maamuzi mbalimbali.
kabla ya PSC, Kamati ya Kitaalamu (Project Technical Committee -PTC) hukutana kupitia, kujadili na kutoa mapendekezo kwa ajili ya maamuzi ya PSC kuhusu utekelezaji wa mradi.
No comments:
Post a Comment