ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 7, 2021

Dkt.ndugulile Ahimiza Uboreshaji Wa Mifumo Mbalimbali Ya Usimamizi Wa Huduma Za Mawasiliano

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imehimiza uboreshaji wa Mifumo mbalimbali ya usimamizi wa huduma za Mawasiliano ili kuhakikisha kunakuwa na Usalama na Ubora wa Huduma Nchini.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea mifumo hiyo kwenye Taasisi ya Udhibiti, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar Es salaam, , Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine E. Ndugulile (Mb) amesema Wananchi wanatarajia kupata huduma bora zenye usalama.

“Upatikanaji wa huduma Bora, za Uhakika na Salama nijambo la msingi sana kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi na Taifa” amesema Mhe. Ndugulile.

Katika ziara hiyo Mhe. Ndugulile alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri K. Bakari na Menejimenti alipotembelea mifumo ya udhibiti wa Mawasiliano.

Dkt. Ndugulile aliipongeza TCRA kwa ubunifu wa kujenga Mifumo Wezeshi kwa huduma mbali-mbali za Mawasiliano Nchini, ambapo alisema uboreshaji wake nimuhimu sana.

Baadhi ya mifumo aliyotembelea Mhe. Waziri ni Mfumo wa Usimalizi na Udhibiti wa Masafa ya Redio na Televisheni na Kituo cha Kuratibu Majanga ya Kimtandao (TZ-CERT). TZ-CERT pia itatoa ushuri wa kitaalam-namna bora wa kudhibiti na kupambana ya majanga mbali-mbali ya Kimtandao kwa Taasisi na makampuni mbali-mbali hapa Nchini.

Mhe. Waziri pia alitembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja ambapo alihimiza TCRA kuendeza kushirikiana na Taasisi zingine zikiwemo za Kiudhibiti kama Bank Kuu ya Tanzania (BOT).

No comments: