ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 5, 2021

MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO AFUNGA MAADHIMISHO SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo, akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Marry Maganga, akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mazingira, Viwanda na Biashara, David Mwakiposa,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, (UNEP) Clara Makenya,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uratibu wa Kampeni ya Mazingira Nchini, Seif Ali Seif,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Mabalozi wa Kampeni ya Utunzaji Mazingira, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Salum,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Mabalozi wa mazingira wakiwemo,wasanii,waandishi wa habari na waigizaji wakifutilia hotuba mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wakifutilia hotuba mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Dar es salaam wakitoa burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Baadhi ya Wanafunzi wakifutilia hotuba mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . Philip Mpango akikata utepe kuzindua andiko la kampeni kabambe ya kitaifa ya uhifadhi na usafi wa mazingira kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akionyesha andiko la kampeni kabambe ya kitaifa ya uhifadhi na usafi wa mazingira kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akibonyeza kitufe akizindua Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Kampeni Kabambe ya Usafi Nchini kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi Mary Maganga andiko la kampeni kabambe ya kitaifa ya uhifadhi na usafi wa mazingira kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akimsikiliza Msanii Mai Zumo,maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, akiangalia baadhi ya Matumizi ya Nishati Mbadala kuongoa Mifumo Ikolojia,alipotembelea banda la UN) kwenye maonyesho ya maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo June 5,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango,amemtaka Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira mhe Seleman Jafo kusimamia utekelezaji wa kampeni kabambe ya kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Dk mpango ametoa wito huo leo June 5,2021 Jijini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa Mazingira nchini.

Dk.Mpango amesema kuwa kumekuwa na mazoea ya upandaji miti kisha kuitelekeza na hivyo Waziri Jafo kajitoe kwa kusimamia miti yote iliyopandwa na tutakupima kulingana na mafanikio hayo.

“Kampeni umeianzisha mwenyewe na utapimwa kwa mafanikio ya hiyo kampeni. Ile miti iliyopandwa siku ya matembezi uhakikishe haifi na mimi nitaikagua”amesema Dk.Mpango

Pia ameitaka Wizara, Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuwahamasisha wananchi utunzajia mazingira, kufuatilia utekelezaji na kutolea taarifa. Juhudi hizo zinajumuisha upandaji miti ya biashara, matunda na dawa.

“Kila kaya ikapande miti katika maeneo yao,kuelimisha umma kuachana na mila potofu zinazoharibu miti na misitu. Halmashauri zikasimamie na kudhibiti uharibu mazingira kwa sababu ya wivu, uonevu au imani potofu.

“Wafugaji waache kuchunga ndani ya mashamba ya mazao ya miti, kukata miti kwenye hifadhi, Serikali za Vijiji ziwajibike kutunza misitu ya asili katika maeneo yao na kusimamia sheria ndogo za utunzaji mazingira.

“Kila Mkuu wa mkoa na katibu tawala miti wapande miti milioni 1.5 kwa mwaka, zamu hii tutakaguana, ahakikishe na kufuatilia kuona miti iliyopandwa inatunzwa na kukua”amesema

Hata hivyo amezitaka Halmashauri na TFS kuongeze jitihada kusimamia mapori na rasilimali, kuzuia moto na kupanga matumizi ya misitu yaweze kuwanufaisha watanzania.

Hata hivyo amesema kuwa Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria Wahalifu wote wa Mazingira kwani Vitendo vya uharibifu wa Mazingira ni dhuluma na ukatili kwa vizazi vijavyo hivyo hawatavumilia uharibifu wowote ule.

Dk. Mpango ametoa wito kwa wafanyabiashara wa gesi ya kupikia kubuni mbinu kusaidia wananchi wa kipato cha chini ili waweze kumudu gharama ya nishati hiyo mbadala.

Awali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo, amesema kuwa maadhimisho ya wiki ya mazingira Tanzania yamefanyika kwa mafanikio katika upandaji miti, maonyesho kuhusu nishati mbadala na mafunzo kwa maofisa mazingira ngazi ya serikali za mitaa na serikali kuu.

Aidha Jafo amesema kuwa watazindua kampeni kabambe ya utunzaji mazingira kwa lengo la kuhamasisha utunzaji na uhifadhi mazingira nchini katika maeneo mbalimbali nchini.

“Lengo la kampeni ni kujenga uzalendo katika utunzaji mazingira na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano kwenye utunzaji mazingira duniani,” amesema Jafo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka, amesema kuwa Mkoa wa Dodoma utahakikisha utunzaji mazingira unakuwa kipaumbele kama ambavyo serikali imekuwa ikisisitiza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mazingira, Viwanda na Biashara, David Mwakiposa,, amesema kazi ya Bunge ni kushauri na kuisimamia Serikali ambapo amesema bado Kuna changamoto ya uchafuzi wa Mazingira katika maeneo ya kuni na mkaa hivyo ni vyema Serikali ikatizama kwa kina matumizi hayo ya Nishati kuu inayotumika ili kuja na Sera nzuri ambayo itaachana na matumizi ya mkaa.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, (UNEP) Clara Makenya,ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa na muamko mkubwa katika suala la utunzaji wa mazingira na wataendelea kuwa bega kwa bega katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika masuala ya utunzaji mazingira.

No comments: