Aliyekuwa
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (kulia ),
akimkabidhi kabrasha, Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Singida, Doroth
Mwaluko katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jana mkoani hapa. ,
Aliyekuwa
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi akizungumza katika
hafla ya kukabidhi ofisi iliyofanyika jana mkoani hapa.
Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Singida, Doroth Mwaluko akizungumza wakati akikabidhiwa ofisi mjini hapa jana
Katibu
Tawala Mpya wa Mkoa wa Singida, Doroth Mwaluko (kushoto) na Aliyekuwa
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi ambaye ameamishiwa
Jijini Mbeya wakisaini nyaraka za makabidhiano ya ofisi jana.
Wakuu wa Idara mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi .
makabidhiano ya ofisi yakiendelea.
Wakuu wa Idara mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi .
Na Mwandishi Wetu, Singida,
Katibu
Tawala mpya wa Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko amekabidhiwa rasmi
ofisi na mtangulizi wake Dkt Angelina Lutambi huku akiahidi kusimamia
kidete elimu ya mtoto wa kike .
Akizungumza
jana kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mwaluko pamoja na mambo mengine
ameomba ushirikiano kutoka kwa watendaji wote mkoani hapa ili kusukuma
kasi ya maendeleo lakini zaidi kuleta ustawi kwenye eneo la elimu na
maboresho ndani ya sekta ya afya.
"Kitaaluma
mimi ni mwalimu,na kipaumbele changu hasa ni masomo ya sayansi natamani
na nitasimamia kuhakikisha watoto wa kike wanasoma masomo haya kwa
mafanikio makubwa,alisema katibu Tawala na akaongeza;
"Kwenye elimu msitarajie kunidanganya na atakaye kwenda kinyume hatutaelewana," alisema
Aidha
kwenye eneo la afya ameomba kila mtendaji kuwajibika ipasavyo ili
matarajio ya wanasingida yazidi kudhihirika kupitia serikali yao
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan
Kwa
upande wake aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Lutambi
ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Mbeya, pamoja na mambo mengine
amemueleza Mwaluko kuwa hali ya uchumi wa Mkoa inaenaendelea kuimarika
siku hadi siku.
Hata
hivyo ameshauri kuwepo kwa msukumo mkubwa na usimamizi kwenye
utekelezaji wa sheria ya fedha za serikali za mitaa hasa kupitia tangazo
la serikali namba 286 la April 5, 2019 ambalo lilielekeza asilimia 10
ya fedha za mfuko wa Wanawake,Vijana na wenye ulemavu zitolewe ipavyo.
No comments:
Post a Comment