ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 6, 2021

RC kafulila aanza kupitia mikataba ya Tanroads

 

Na Samirah Yusuph - Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila  ameitisha mkataba 31ya ujenzi na ukarabati wa barabara iliyotolewa na Tanroads msimu wa fedha 2020/2021 ili kuweza kuikagua na kufanya tathimini ya utekelezaji wa mikataba hiyo pamoja na kutathimini ubora wa miundombinu kuendana na thamani ya Fedha zilizotolewa.

Kafulila ameyaeleza hayo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara mkoani humo  June 5, 2021 baada ya kubainishwa kuwa miundombinu ya barabara ninchangamoto katika kukuza sekta ya biashara na usafirishaji wa malighafi kwa ajili ya mauzo na uzalishaji wa bidhaa.

Amebainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa barabara hizo kujengwa chini ya kiwango hivyo kuamua kupitia mikataba hiyo yenye thamani ya tsh17 bilioni ili kufanya mapitio kubaini thamani ya kila barabara kuendana na ubora wake pamoja na marekebisho ya msimu huu wa fedha.

"Shida ya barabara ipo, lazima ujenzi wa barabara uwe wa viwango na maeneo ambayo mkandarasi alijenga chini ya kiwango lazima arudie...

Pengine tatizo limeanzia wakati wa kusaini mkataba pale pale tunahitaji kuona kila mkataba ulifanya kazi wapi, ukaguzi unaanzia Tanroads na tutakwenda hadi Tarura ili kujiridhisha".

Aidha Kafulila amewataka watumishi wa serikali kuwa ni daraja la kutengeneza fulsa kwa wajasiliamali na kujielekeza zaidi katika kuhakikisha wanafikiria namna ya kuongeza tija ya uzalishaji kwa wafanyabiashara na wajasiliamali wadogo.

Wakiwasilisha mapendekezo yao baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicho wameomba kuboreshewa mazingira ya kufanyabiashara mkoani humo ikiwa ni pamoja na kutengenezewa mfumo rafiki utakao wawezesha kuzifikia kwa wepesi mamlaka zinazohusika na ubora wa bidhaa.

"Changamoto tuliyo nayo ni katika kutafuta Bland na TBS hivyo maafisa biashara wageuke kuwa madaraja ya kuongeza thamani ya bidhaa za wafanyabiashara wadogo katika kukuza soko na kuwaongoza namna ya kuongeza thamani ya bidhaa," alisema katibu wa chama cha wanawake wafanyabiashara mkoa wa Simiyu (TWCC) Happy severine.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Simiyu John Sabu ameeleza kuwa Malimbikizo ya madeni ya wafanya biashara katika halmashauri za wilaya ni sababu inayopelekea wazawa kushindwa kufanya kazi na halmashauri mkoani humo na kuwaachia wageni waweza kuchukua tenda hizo.

Mwisho.

 

No comments: