Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari
akibonyeza kitufe kama ishara ya kuuzindua rasmi mfumo wa kielektroniki
wa utoaji wa vibali kwa ndege zinazotoka nje ya nchi na kutua ama
kupita katika anga la Tanzania.
Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezindua mfumo wa kielektroniki wa
utoaji wa vibali kwa ndege zinazotoka nje ya nchi na kutua ama kupita katika anga la Tanzania.
Mfumo
huu unarahisisha maombi pamoja na utoaji wa vibali kutoka masaa 48 ya
awali hadi masaa mawili. Vilevile mfumo huu unampa nafasi muombaji wa
vibali kunakili na kutoa nakala ya kibali chake popote alipo. Mfumo huu umetengenezwa na wataalamu wa ndani wa Mamlaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari pamoja na maofisa wa TCAA wakitazama mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa vibali kwa ndege zinazotoka nje ya nchi kuingia katika anga la Tanzania mara baada ya kufanya uzinduzi huo .
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari
akizungumza na waadhishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mfumo wa
kielektroniki wa utoaji wa vibali kwa ndege zinazotoka nje ya nchi
kuingia katika anga la Tanzania uliofanyika katika ofisi za TCAA jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA),
Daniel Malanga akielezea namna waombaji wa vibali watakavyokuwa
wakiomba vibali kupitia mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa vibali kwa
ndege zinazotoka nje ya nchi na kuingia nchini uliozinduliwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea
No comments:
Post a Comment