Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirikisho la michezo la mashirika ya umma na kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo. Septemba 30,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhiwa zawadi ya ngao ya heshima kutoka kwa viongozi wa Shirikisho la michezo la mashirika ya umma na kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) akiwa mlezi wa shirikisho hilo mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo. Septemba 30,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhiwa mavazi ya michezo kutoka kwa viongozi wa Shirikisho la michezo la mashirika ya umma na kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo. Septemba 30,2021.
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais ametaja Michezo kama njia ya kuleta umoja na undugu katika maeneo ya kazi pamoja na kuondokana na maradhi mbalimbali. Amesema kupitia michezo ndio kunaweza pia kukabiliana na Uviko 19 pamoja na kutoa elimu ya kupata chanjo ya ugonjwa huo.
Makamu wa Rais ametoa rai kwa Shimmuta kutumia michezo wanayoisimamia kutoa elimu ya utunzaji mazingira. Amesema yapo maeneo mengi yanayohotaji upandaji miti pamoja na usafi wa mazingira hivyo Shimmuta inapaswa kuwa chachu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa vitendo.
Aidha Makamu wa Rais ameiasa SHIMMUTA kufanya michezo itakayotoa mchango katika jamii kama vile Riadha zinazofanywa kwa lengo la kupata fedha na kusaidia katika huduma za kijamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shimmuta, Hamis Mkanachi amesema changamoto inayoikabili Shimmuta ni ukosefu wa udhamini katika mashindano yanayoandaliwa pamoja ushiriki mdogo wa Mashirika, Kampuni na taasisi katika michezo hiyo.
Mashindano ya Shimmuta mwaka 2021 yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro katikati ya mwezi Novemba.
No comments:
Post a Comment