Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk.John Jingu,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Anthony Mtaka,akitoa salamu za Mkoa wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO) Dkt. Lilian Badi,akielezea malengo ya Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua taarifa ya mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa Mkutano wa Mwaka wa NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya heshima kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa Mkutano wa Mwaka wa NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna, DodomaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia Mipango na Vipaumbele vya Kitaifa katika kutekeleza majukumu na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rais Samia amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Mkutano wa Mwaka wa Mashirika hayo.
“Napenda kuyaelekeza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwa na mpango mkakati wa Maendeleo utakaokwenda sambamba mpango wa Taifa wa miaka mitano,” amesema na kuongeza; huko nyuma Mashirika mengine yalikuwa yakifanya kazi kulingana na matukio, ukianzishwa mpango wa mazingira Mashirika yanakimbilia huko ili kushawishi fedha za wafadhili. Ni imani yangu mtajipanga upya kufanya kazi kwa ufanisi” amesema Mhe. Samia.
Aidha, ameyataka Mashirika hayo kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao na miradi mbalimbali kwa kuzingatia tamaduni, mila na desturi za nchi.
Mashirika ya ndani pia wametakiwa kupunguza utegemezi kwa wafadhili na wadau wa Maendeleo kutokana na mabadiliko ya Sera na Agenda za wadau hao bali waanzishe miradi ya kuwatengenezea fedha kwa kushirikiana na Serikali.
Aidha ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhamasisha zoezi la Sensa likatalofanyika nchini mwaka 2022 ili Taifa liweze kujiletea Maendeleo katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Rais kwa uongozi wake mahiri uliowezesha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kupata uongozi.
Ameongeza pia, kupitia mkutano huo Mashirika hayo yamepata semina elekezi kuhusu sheria, kanuni na miongozo hivyo ni matumaini kuwa sasa wamefahamu wanatakiwa kufanya nini.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Lilian Badi amesema Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yatazingatia sheria, kanuni na miongozo pamoja na kushirikiana na Serikali ili kutoa mchango wenye tija nchini.
No comments:
Post a Comment