Meneja
wa Kampuni ya GOPA CONTRACTORS Godfrey John, amewaomba radhi Wakulima
katika Skimu ya Endagaw kwa kuchelewa kuanza ujenzi wa Miundombinu ya
Mifereji na Ukarabati wa Bwawa kwa zaidi ya miezi miwili.
Akizungumza
katika kikao kilichowashirikisha, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Bi Janeth
Mayanja, watendaji wa Tume na Wakulima wa Skimu hiyo, Meneja wa kampuni
ya GOPA CONTRACTORS Bw, Godfrey John amekiri kampuni yake kushindwa
kuanza shughuli za ujenzi katika Skimu hiyo kwa mujibu wa mkataba wa
makubaliano na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kwamba zoezi la ujenzi
litaanza hivi karibuni kwa ubora na viwango vilivyoainishwa kwenye
mkataba baada ya kutatua changamoto zilizoikabili kampuni yake.
Mhandisi
wa Tume ya Taifa Umwagiliaji Bw, Juma Hamsini, ametoa onyo kali kwa
mkandarasi huyo na kuongeza kuwa endapo kampuni yake itarudia kutenda
kosa kama hilo, Tume ya taifa ya Umwagiliaji itaiweka kampuni hiyo
katika orodha ya makampuni yanayotiliwa shaka kiutendaji hali
itakayosababisha kampuni hiyo kukosa fursa ya ujenzi wa Miradi ya
Miundombinu ya Umwagiliaji inayoratibiwa na Tume.
Kwaupande
wake Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi, Janeth Mayanja, amemtaka Mkandarasi
huyo kujenga Miundombinu kwa viwango na ubora kwa mujibu wa mkataba na
kwamba atafuatilia ujenzi wa Mradi huo kwa karibu hadi utakapo kamilika.
Tume
ya Taifa ya Umwagiliaji ilisaini makubaliano na kampuni ya Gopa
Contractors ya jijini Dar es Saalam, kujenga Mfereji mpya wenye urefu wa
Mita Elfu mbili na Mianne (2,400) sanjari na kuongeza urefu mfereji wa
zamani kwa kujenga Mita Miasaba na Sabini (770) pamoja na kuondoa Tope
ndani ya bwawa linalotumika kumwagilia Skimu ya Endagaw.
Mkataba
wa ujenzi wa miundombinu hiyo baina ya Tume na Mkandarasi Gopa
Contractors ni wa zaidi ya Shilingi Milioni Miatisa Themanini.( Milioni
980) na ulisainiwa tarehe 31.08. 2021.
Bakari
Khamis – Diwani wa Endagaw akiwaonyesha Wahandisi wa Tume changamoto
zilizopo katika Bwawa la Endagaw linalotumika kumwagilia Skimu ya
Endagaw.
No comments:
Post a Comment