Na John Walter-Babati
Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema kilichotokea Halmashauri ya Mji wa Babati alitarajia kwa kuwa hawakupokea ushauri wake.
Akizungumza katika baraza maalum la Madiwani kujadili Hoja 35 za CAG katika Halmashauri hiyo, Twange amesema aliwahi kuwaandikia Barua kuwataka kubadilisha Baadhi ya masuala lakini hawakuzingatia na ndio matokeo yake yameonekana baada ya kupata hati yenye mashaka.
Aidha kwenye vikao vya Halmshauri hawaishirikishi ofisi yake.
Amesema kuna wakati hata Katibu tawala wa wilaya anatolewa nje Kisha wanaendelea na majadiliano.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere.
No comments:
Post a Comment