ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 15, 2023

JUMLA YA WANAFUNZI 342,933 WAMESAJILIWA KATIKA MFUKO WA NHIF.


NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha kuwa Serikali kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mpaka kufikia Machi 2023 umeshasajili jumla ya wanafunzi 342,933 ikiwemo wa Shule za msingi, Sekondari na Vyuo vya Kati unaotoa nafasi kwa wananchi hao kupata matibabu bila malipo katika vituo vyote vinavyotoa huduma za NHIF.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Juni 15, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Lucy John Sabu, Bungeni Jijini Dodoma.

"Hadi kufikia Machi 2023, Mfuko umeshasajili jumla ya wanafunzi 342,933 ikiwemo wa Shule za msingi, Sekondari na Vyuo vya Kati."

Ameendelea kusema, zoezi hili la kusajili wanafunzi ni endelevu kupitia shule na vyuo ili kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi kuingia katika mfuko huo ili wapate huduma bila matibabu, huku akisisitiza kuwa, wanafunzi watatakiwa kuchangia shilingi 50,400 ili kupata bima ya matibabu.

No comments: