Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Makame (mwenye tai nyekundu) akisikiliza ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na mabaharia wakati alipotembela na kukagua mabanda hayo.
Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Makame akifuatilia ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani yaliyofanyika katika uwanja wa furahisha jijini Mwanza
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Shekilage akitoa salamu kwa mabaharia kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Amos Makala
Msimamizi mkuu wa bandari Zanzibar Sheikha Mohamed akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani
Mjumbe wa bodi ya shirika la meli Tanzania TASAC King Chiragi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani
Mwakilishi wa kampuni za huduma za meli ndug Anselm Namala akiendelea kupata taarifa katika mabanda ya maonyesho ya siku ya mabaharia duniani.
Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Makame akisikiliza ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na mabaharia wakati alipotembela na kukagua mabanda hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu wakifuatilia ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani.
Wadau mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa maadhimisho ya mabaharia duniani.
Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Makame amezitaka taasisi zinazosimamia mabaharia hapa nchini ziweze kuboresha maslahi ya mabaharia hao ili kazi hiyo iweze kua yenye tija kama zilivyo kazi nyingine.
Waziri Makame ameyasema hayo Alhamis Juni 22, 2023 wakati akifungua maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani yanayofanyika kitaifa jijini Mwanza akimwakilisha Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman.
"Nikubaliane na waliosema na mimi nalisema hii kwa sababu nimeiona na nimeisikia maslahi duni ya mabaharia zipo taasisi hapa ambazo zinasimamia mabaharia naomba hili mlichukue mwenyekiti amesema chungu kipo jikoni lakini lisikawie basi",amesema.
Katika hatua nyingine Waziri Makame amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini ikiwemo ujenzi wa meli mpya ya MV. Mwanza pamoja na ukarabati wa meli ya MV. Mapinduzi II.
Aidha pia Mh. Makame pia ameongeza kwa kuitaka jamii iweze kuondokana na dhana potofu ambazo zimekua zikiihusisha kazi ya baharia na uhuni kwani kazi hiyo husomewa na fani kama zilizo fani nyingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ambae aikua akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. Amosi Makalla amesema serikali ya awamu ya sita imekua ikifanya shughuli mbalimbali za maendeleo katika sekta ya bahari na maziwa ambapo mwa mkoa wa mwanza serikali imetoa kiasi cha silingi bilioni 21 kwa ajili ya ujenzi wa vizimba vya samaki huku pia ikitekeleza mradi wa ujenzi wa meli mya ya MV. Mwanza ambayo imegharimu kiasi cha billion 111 na kukamilika kwa miradi hiyo kutaibua fursa ya ajira kwa watu mbalimbali hapa nchini.
Naye mjumbe wa bodi ya wakurugenzi TASAC Captain. King Chiragi amesema wao kama TASAC wanaridhika na namna serikali inashughulikia tasnia ya bahari kwani serikali imekuwa ikitunga sera ambazo zimekuwa zikilenga kuimarisha ustawi wa baharia
Aidha amewaomba wananchi wote waweze kuwaheshimu mabaharia wote hapa nchini kwani wamekuwa wakijtoa sana katika kulinda ustawi wa jamii.
Katibu Chama cha Mabaharia Zanzibar, Ally Mzee ambaye amezungumza kwa niaba ya mabaharia, amesema kada hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika, maslahi duni, mazingira rafiki kazini hususani kwa wanawake pamoja na vyama kushindwa kuwatetea mabaharia wanapokumbana na changamoto kazini.
Maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani yanafanyika kitaifa katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kuanzia Juni 22-25, 2023 ambapo yataambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji elimu usalama majini, kufanya usafi katika fukwe za Ziwa Victoria pamoja na mbio ya riadha itakayowashirikisha mabaharia yakiambatana na kauli mbiu isemayo “Miaka 50 ya Marpol, uwajibikaji unaendelea”.
No comments:
Post a Comment