Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Jesca Leba ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuwezesha upatikanaji wa Kliniki ya Himofilia na Selimundu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma - Maweni.
Dkt. Jesca ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Prof. Pascal Rugajo katika uzinduzi rasmi wa Kliniki hiyo amesema uwepo wake katika kanda ya magharibi utasaidia wagonjwa kupata huduma karibu badala ya kuzifuata mbali.
"Uzinduzi huu ulitanguliwa na mafunzo ya namna ya kuwatambua na kuwahudumia wagonjwa wa Himofilia yaliyotolewa na wataalamu kutoka MNH kwawatoa huduma na wataamu wa hospitali ya maweni na hospitali za jirani, jambo ambalo litawasaidia kumudu uendeshaji wa kliniki hii" amesema Dkt. Binagi.
No comments:
Post a Comment