ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 23, 2023

POLISI KUTOKA UJERUMANI NA THAILAND WABADILISHA UZOEFU KATIKA MASWALA YA POLISI JAMII


Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi-Dar es Salaam

Askari Polisi kutoka Ujeruman na Thailand wametoa uzoefu wao katika maswala ya Polisi Jamii na namna ambavyo wanatoa huduma kwa jamii katika mataifa hayo ambayo yamejikita zaidi katika maswala ya Polisi Jamii.

Akiongea mara baada ya mafunzo hayo Profesa Krisanaphong Poothakool, kutoka Thailand amesema Polisi awezi kufanya kazi mwenyewe bila kushirikisha jamii ambapo amebainisha kuwa Polisi akiamiwa na jamii ananafasi kubwa ya kupata taarifa.

Ameeendelea kusema kuwa Polisi watanzania wanayonafansi ya kufanya jitihada Zaidi katika maswala ya Polisi jamii wanayofanya kupata kile wanachokita katika kutokomeza uhalifu.
Nae kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP URICH MATEI ambae amemwakilisha kamishina wa kamisheni ya Polisi Jamii CP FAUSTINE SHILOGILE amesema dira ya Polisi kwa sasa chini ya Mkuu wa Jeshi ni kushirikisha jamii katika kukabiliana na uhalifu Katika jamii ambapo ameongeza kuwa watumishi wa serkali za mitaa kushirikiana na askari kata.

SACP Matei amewataka maofisa wanafunzi waliopata elimu hiyo na uzorfu kutoka kwa Polisi wa Thailand na Ujerumani kutumiwa vyema elimu waliyo ipata Kwenda kutoa huduma bora Zaidi kwa wananchi wanao litegemea Jeshi la Polisi.
Kwa upande wake Bw. Bw Karl-Peter Schönfisch amemshukuru mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania IGP Camillus Wambura kwa matokeo chanya wa mfumo wa Polisi jamii ambapo amesema wao wamejifunza vitu vizuri kutoka Jeshi la Polisi Tanzania kwa namna wanavyoshirikisha jamii kutatua uhalifu ambapo amebainisha kuwa wao wamekuwa wakishirikisha jamii bila ya kuwa na kamisheni inayohusika na Polisi jamii katika maswala ya Polisi jamii.

Nae mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi dar es salaam Daktari Lazaro Mambosasa amewashukuru askari hao kwa kubadilisha uzoefu licha ya kuwa wao wako mbele kiteknolojia katika kukabiliana na uhalifu ambapo amebainisha kuwa wamejifunza vitu vingi ambavyo vtakuwa na faida kwa jamii na taifa kwa ujumla.

No comments: