ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 24, 2023

TCDC YATUNUKIWA CHETI CHA PONGEZI KWA KUANDAA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA ULIOKIDHI VIWANGO



WAZIRI wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,George Simbachawene akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikataba ya huduma kwa wateja na taasisi za umma hafla iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejeimenti ya Utumishi wa Umma na Utwala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Raslimaliwatu, Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Bw.Gabriel Mwita, Cheti cha pongezi kwa TCDC kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja uliokidhi vigezo katika hafla ya uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa mteja iliyofanyika Juni 23,2023 jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali Wizara na Taasisi za Serikali wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejeimenti ya Utumishi wa Umma na Utwala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa mteja iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejeimenti ya Utumishi wa Umma na Utwala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi za Serikali waliopatiwa vyeti vya pongezi kwa kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja uliokidhi vigezo katika hafla ya uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa mteja iliyofanyika leo Juni 23,2023 jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna-DODOMA

Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imekuwa miongoni mwa Taasisi chache za Serikali zilizotunukiwa cheti cha pongezi kwa kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja uliokidhi vigezo vinavyotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR – UTUMISHI).

TCDC imeitunukiwa cheti hicho kilichoandaliwa na OR – UTUMISHI Juni, 23,2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikataba ya huduma kwa mteja ya taasisi mbalimbali za Serikali ikiwa ni siku ya kilele cha wiki ya utumishi wa Umma.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejeimenti ya Utumishi wa Umma na Utwala Bora, Mhe. George Simbachawene, amezipongeza taasisi zilizoandaa mikataba hiyo kwa kuzingatia vigezo vilivyotolewa na kusisitiza kuwa yote yaliyoelezwa katika mikataba hiyo yazingatiwe ili wananchi waweze kupata huduma bila usumbufu.

Waziri Simbachawene amesema unakusudia kuwawezesha wateja kuelewa majukumu ya taasisi husika, huduma zinazotolewa, haki na wajibu katika kupata huduma, taratibu za kupata huduma na hivyo kuimarisha uhusiano kati ya taasisi na wateja wake.

“Mkataba wa huduma kwa mteja ni muhimu sana kwani unasaidia Serikali kutoa huduma bora na hivyo wananchi kuifurahia na kuipenda Serikali yao kwa kuwa inawaletea maendeleo. Ninazielekeza Taasisi zote za Serikali ambazo bado hazina Mkataba wa Huduma kwa mteja kuhakikisha zinaandaa mkataba huo mara moja kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Ofisi yangu,” amesema Waziri Simbachawene.

Hata hivyo Waziri Simbachawene amezitaka Taasisi zote za umma kuhakikisha Mikataba hiyo inatekelezwa kikamilifu na kuondoa urasimu katika utoaji wa huduma unaosababisha usumbufu na wakati mwingine wananchi kukosa huduma.

No comments: