ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 9, 2023

WAZIRI DKT. CHANA AKAGUA JENGO LA WIZARA ASISITIZA KUKAMILIKA KWA WAKATI


Na shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Juni 8, 2023 amekagua ujenzi wa Jengo la wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma na kuridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika jengo hilo.

Mhe. Chana amemtaka Mkadarasi wa Jengo hilo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi ujenzi huo ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Naye Mhandisi wa Jengo hilo Bw. Omari Saidi amesema kuwa wanahakikisha jengo hilo linaendelea kujengwa kwa viwango, kasi na kuahidi kulikabidhi Oktoba mwaka huu 2023 kama Mkataba unavyosema.

Awali Mhe. Chana alitembelea eneo la Ujenzi wa Uwanja wa Dodoma ambapo ameshuhudia baadhi ya vifaa vya ujenzi vikiwa tayari katika eneo hilo kuanza ujenzi.

No comments: