ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 23, 2023

WAZIRI DKT. CHANA AKARIBISHA MATAIFA KUJIFUNZA KISWAHILI


Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Tanzania Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana akizungumza katika hafla ya kuyakaribisha Mataifa mbalimbali kujifunza lugha ya Kiswahili kupitia Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Balozi za Tanzania Ulimwenguni.
Na Brown Jonas
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewakaribisha Mataifa mbalimbali kujifunza lugha ya kiswahili kupitia Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Balozi za Tanzania Ulimwenguni ili kufikia lugha hiyo ambayo ni miongoni mwa lugha kubwa Duniani.

Mhe. Chana amesema hayo Juni 22, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi "Tumia Akili Game" ambayo itatumia maneno ya kiswahili katika Taasisi za Elimu nchini Italia ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya miaka 500 ya mchoraji maarufu wa nchi hiyo Mr. Pietro Vannucci.
"Ninatoa pongezi nyingi kwa Ubalozi wa Italia hapa nchini kwa kushirikikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza lugha ya Kiswahili kupitia "Tumia Akili" mchezo ambao utatumia silabi za kiswahili na kuunda maneno ya lugha hiyo ambayo inakua kwa kasi Duniani na kuzungumzwa na watu Milioni 500 Ulimwenguni" amesema Mhe. Chana.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali kujifunza lugha ya Kiswahili huku akiwaalika wananchi wa Italia kujifunza Kiswahili kupitia Kituo kilichopo nchini humo.

Kwa upande wake Balozi wa Italia hapa nchini Bw. Marco Lombard amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania kukuza lugha ya kiswahili.












No comments: