ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 14, 2024

ALI KIBA,MARIOO,HARMONIZE JUKWAA MOJA MKESHA WA MWENGE MUHEZA

 
Na Oscar Assenga,Muheza
WASANII Nguli wa Mziki wa BongoFleva hapa nchini Alikiba ,Marioo na Harmonize wametajwa kuwa miongoni mwa wasanii 10 wakubwa ambao watauwasha moto wilayani Muheza wakati wa Mkesha wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kesho April 15,2024

Mkesha huo wa mwenge wa Uhuru utakuwa chini ya Udhamini wa Rais wa Crown Media Ali Kiba na utafanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza huku wananchi mbalimbali wakikaribishwa kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye eneo la Kivutio cha Utalii cha Magila wilayani Muheza Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah alisema kwamba maandalizi ya mbio hizo yamekamilika na wasanii hao wamekwisha kuingia wilayani humo kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa mji huo.

“Maandalizi ya Mwenge wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanaendelea vizuri na tunategemea tutaupokea katika Kijiji cha Mkanyageni na utakimbizwa katika miradi mbalimbali iliyopangwa hivyo nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kuulaki kila utakapokuwa umepita”Alisema

Katika Jukwaa hilo la mkesha wa Mwenge Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma ambaye pia ni Naibu Waziri wa Michezo,Sanaa na Utamaduni atakuwa sehemu ya wasanii ambao wanatumbuiza kwenye tamasha hilo.

Wasanii wengine amba watalipamba jukwaa hilo licha ya hao ni Bilinass,Ommy Dimposi,Maua Sama,Dulla Makabilla,Chino,Contawa ambao watatoa burudani kwa wakazi wa mji wa Muheza katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru utakaofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani humo.

Akizungumza kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mwana FA alisema mkesha wa mwenge wa uhuru mwaka huu utakuwa babu kubwa na utafunika maeneo mengine ambazo utakuwa umekesha kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

“Lakini kubwa tunajivunia aina ya miradi ni mizuri na mikubwa kikubwa nitoe shukrani kwa Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutuwezesha kuwa na miradi hiyo kazi yetu ni kuendelea kuomba na uwepo usimamizi wa fedha zinazokuja Muheza haziwezi kuingia shimboni bali zinatumika kutatua changamoto za wananchi”Alisema

Hata hivyo kwa upande wake Msanii Maua Sama ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Mazingira alishukuru kwa kupata nafasi ya kuwa balozi pamoja na yote,vijana wana mambo mengi wanakwenda kufanya pamoja na watashirikiana.

Hata hivyo kwa upande wake Msanii Mwijaku alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa namna anavyosimamia ilani ya CCM na maono ya Rais Samia kuongozi wa kweli ambaye hupigania uwekezaji wa maendeleoo na wanahitaji maendeleo ya kweli na sio viongozi wenye maneno maneno.

Mwijaku pia alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu na Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah kwa kuendelea kuifungua nchi kwa miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo.

No comments: