Advertisements

Sunday, April 14, 2024

MAREKANI YASEMA HAITASHIRIKI KATIKA MASHAMBULIZI YOYOTE DHIDI YA IRAN


Katika mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumamosi usiku, Rais wa Marekani Joe Biden aliweka wazi kuwa Marekani haitashiriki katika mashambulizi yoyote dhidi ya Iran - huku akisisitiza "dhamira ya dhati ya Marekani kwa usalama wa Israel," Afisa mwandamizi wa Ikulu ya White House, ameiambia CNN.

Rais Biden alimwambia Netanyahu kwamba anapaswa kuzingatia matukio ya Jumamosi usiku kama "ushindi" kwani mashambulizi ya Iran hayakufanikiwa kwa kiasi kikubwa, na badala yake alionyesha "uwezo wa ajabu wa Israeli wa kujilinda na kushinda mashambulizi ambayo hayajawahi kutokea."

Marekani ilitathmini kuwa karibu ndege zisizo na rubani na makombora - ikiwa ni pamoja na zaidi ya makombora 100 ya balistiki - yaliyorushwa na Iran yalikuwa yametupwa kutoka angani. Hakuna kombora la kusafiri lililoleta madhara.

Hakujawa na ripoti za majeruhi moja kwa moja kutokana na mashambulizi ya Iran, kwa mujibu wa idara ya dharura ya Israel, ingawa ilisema msichana wa miaka 7 alijeruhiwa vibaya na kipande cha chuma kilichotoka kwenye makombora la kujihami la Israel.

Habari za shambulio hilo zilipoibuka, makazi ya kujihifadhi raia yalifunguliwa katika mji wa kaskazini mwa Israel wa Haifa na mikusanyiko mikubwa ya watu kupigwa marufuku. Israeli ilifunga anga yake, kama ilivyofanya karibu na Jordan, Iraqi na Lebanon. Kufikia Jumapili asubuhi Israeli na Jordan zilifungua tena anga zao.

Timu ya CNN mjini Jerusalem iliweza kusikia milipuko na ving'ora huku milipuko ya sauti ikifanyika mapema Jumapili asubuhi saa za huko.

IRAN YAONYA DHIDI YA KULIPIZA KISASI KWA ISRAEL

Kwa upande wake Iran imesema, itajibu mashambulizi makubwa zaidi katika ardhi ya Israel iwapo Israel italipiza kisasi dhidi ya ndege isiyo na rubani ya Tehran na mashambulizi ya makombora.

"Jibu letu litakuwa kubwa zaidi kuliko hatua ya kijeshi ya leo usiku ikiwa Israeli italipiza kisasi dhidi ya Iran," mkuu wa majeshi wa Iran, Meja Jenerali Mohammad Bagheri aliiambia TV ya serikali.

Meja Jenerali Bagheri ameongeza kuwa, Tehran imeonya kwamba vituo vya Marekani vitalengwa ikiwa Washington itaunga mkono kulipiza kisasi kwa Israel.

Kufikia sasa, Rais wa Marekani Joe Biden amesema anataka kuratibu "mwitikio wa kidiplomasia wa pamoja" kwa shambulio la Iran katika mkutano wa kundi la G7 la mataifa tajiri anaonuia kuuitisha Jumapili.

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hossein Salami pia alitahadharisha kuwa Tehran itajibu kwa vitendo shambulio lolote la Israel dhidi ya maslahi yake, maafisa au raia wake.

CHANZO: K-VIS BLOG

No comments: