Advertisements

Saturday, April 13, 2024

RAIS SAMIA AKEMEA VIONGOZI WANAOICHONGANISHA SERIKALI NA JAMII



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024. Hayati Sokoine alifariki tarehe 12 Aprili, 1984 kutokana na ajali ya gari iliyotokea Wami Dakawa Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Ibada Maalum ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo ya Misa Takatifu imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mama Fatma Karume Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume ambaye pia alihudhuria Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo ya Misa Takatifu imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo ambaye pia alihudhuria Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo ya Misa Takatifu imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
  

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na baadhi ya viongozi wasiotambua dhamana walizonazo ambao hutumia nafasi zao kuleta uchonganishi badala ya kuleta maelewano kati ya Serikali na jamii.
Rais Samia amesema hayo, wakati akizungumza katika Kumbukizi ya Miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, akiwasisitiza viongozi kuiga mfano wa Hayati Sokoine kwani alikemea jambo hilo kwa maneno na vitendo.

Rais Samia amesema Hayati Sokoine alitumia utashi wake wa hali ya juu kuimarisha mahusiano kati ya Serikali na jamii aliyoiongoza na kuiwakilisha vyema jamii ya Wamaasai.

Rais Samia amewataka viongozi wa sasa na wajao kutambua kuwa uamuzi ukifanyika ndani ya Serikali, ni wajibu watekeleze uamuzi huo kama ulivyofikiwa hata ikibidi wao wawe mfano kwa wengine kama Hayati Sokoine alivyofanya.

Kuhusu umuhimu wa elimu kama ulivyopewa kipaumbele na Hayati Sokoine, Rais Samia ametoa wito kwa wazazi kutumia vyema fursa ya miundombinu bora ya Elimu inayojengwa na Serikali kuwa peleka watoto shule.

Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kuendelea kutunza kumbukumbu za viongozi wa Taifa na kuhakikisha habari zao zinawafikia vijana wengi zaidi kupitia njia za kisasa.

Rais Samia ametumia fursa hiyo pia kutoa pole kwa waathiriwa wote wa mafuriko na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kufanya kila linalowezekana kuepusha madhara zaidi na kuwataka pia wananchi kusikiliza maelekezo ya tahadhari zinazotolewa.

Pia Rais Samia amesema baada ya mvua hizo na hali ya kawaida kurejea, Serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu za mafuriko hayo ili kuepusha madhara makubwa kwa siku zijazo.


Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

No comments: