ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 12, 2024

WAZIRI MKUU AWASILI JIJINI ARUSHA KUSHIRIKI KUMBUKUMBU YA MIAKA 40 YA KIFO CHA HAYATI EDWARD SOKOINE




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  Aprili 11, 2024 amewasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kisongo jijini Arusha ambapo kesho Aprili 13, 2024 atashiriki katika Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine itayofanyika Moduli.

Mheshimiwa Majaliwa amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Loy Thomas Ole Sabaya.

No comments: