Wednesday, May 29, 2024

IFAD KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI YA KILIMO NA UVUVI NCHINI


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akipeana mikono na Makamu wa Rais Mshiriki anayeshughulikia miradi katika Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dkt. Donal Brown mara baada ya kikao kati ya Tanzania na Mfuko huo, kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jijini Nairobi nchini Kenya. Dkt. Mwamba anamwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika Mikutano hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akizungumza katika kikao kati ya Tanzania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kuhusu ushirikiano kati ya nchi na Mfuko huo, kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya. Dkt. Mwamba anamwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika Mikutano hiyo.
Makamu wa Rais Mshiriki anayeshughulikia miradi katika Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dkt. Donal Brown (katikati), akizungumza katika kikao kati ya Tanzania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kuhusu ushirikiano kati ya nchi na Mfuko huo, kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba ambaye anamwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika Mikutano hiyo.
Makamu wa Rais Mshiriki anayeshughulikia miradi katika Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dkt. Donal Brown (katikati), akizungumza katika kikao kati ya Tanzania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kuhusu ushirikiano kati ya nchi na Mfuko huo, kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba ambaye anamwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika Mikutano hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akimsikiliza Makamu wa Rais Mshiriki anayeshughulikia miradi katika Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dkt. Donal Brown, katika kikao kati ya Tanzania na Mfuko huo, kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), inayofanyika Jijini Nairobi, nchini Kenya, ambapo Dkt. Mwamba anamwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika Mikutano hiyo.

Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje kutoka Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Bw.Yusuf Ibrahim Yussuf (kulia) na Kamishna Msaidizi wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule wakifuatilia kwa karibu masuala mbalimbali katika kikao kati ya Tanzania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), kilichofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jijini Nairobi nchini Kenya. Katika Mikutano hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba anamwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) na Makamu wa Rais Mshiriki anayeshughulikia miradi katika Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dkt. Donal Brown (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil na Mkurugenzi, Kitengo cha Afrika Mashariki na Kusini katika Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bi. Sara Mbago-Bhunu baada ya kikao kati ya Tanzania na Mfuko huo, kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jijini Nairobi nchini Kenya. Dkt. Mwamba anamwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika Mikutano hiyo.



Na. Ramadhani Kissimba na Farida Ramadhani, WF - Nairobi
Serikali imeushukuru Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kilimo na uvuvi nchini.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, baada ya kikao kati ya Tanzania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.
Dkt. Mwamba alisema Mfuko huo umekuwa ukiendelea kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo na uvuvi nchini kwa pande zote mbili za Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar).
“Tutaongea na wenzetu wa Sekta husika kuainisha miradi ambayo Serikali inataka iingie kwenye program mpya itakayoanza Januari, 2025 na kuiwasilisha Tume ya Mipango ili ifanyiwe uchambuzi kabla ya kuwasilishwa kwenye mfuko huo.”, alisema Dkt. Mwamba.
Aidha Dkt. Mwamba alieleza kuwa kutokana na changamoto ya huduma ya fedha inayowakabili wakulima wengi nchini hasa wale wadogo, Serikali pamoja na IFAD wamekubaliana kuwa katika program mpya itakayoanza Januari, 2025 kwa kuingiza miradi ambayo itasaidia upatikanaji wa fedha kwa wakulima wadogo ili waweze kuendeleza miradi yao ya kilimo na miradi ambayo inawagusa wananchi kwa moja.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho, Dkt. Mwamba alisema kuwa ili kuimarisha sekta ya uvuvi nchini, suala la uhifadhi wa mazingira limetiliwa mkazo ili kulinda mazalia ya samaki ambayo yanaweza kuharibiwa wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema kwa kuwa program hiyo ya IFAD inahusisha uwepo wa meli kubwa za uvuvi, upembuzi yakinifu unaendelea kufanywa kuhusu kulinda mazingira ya mazalia hayo ya samaki ili wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo isiathiri sekta ya uvuvi nchini.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais Mshiriki anayeshughulikia miradi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dkt. Donal Brown, alisema IFAD kupitia miradi yake mbalimbali inalenga kuinufaisha jamii hasa kwa wale wanaoishi vijijini ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu inayohusiana moja kwa moja na kilimo cha biashara.
‘’Miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), inalenga moja kwa moja kusaidia jamii nzima zilizopo vijijini kupitia miradi mikubwa mbalimbali inayotekelezwa na Mfuko, hasusan ile ya maji ambayo inasaidia kurahisisha na kuendeleza kilimo cha kibiashara.’’ Alisema Dkt. Brown.
Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) umekuwa ukifanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuendeleza sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi nchini ili kufikia uzalishaji wa juu, endelevu na kibiashara. Ikiwa ni pamoja na kuongeza mapato ya wakulima wadogo na kuboresha upatikanaji wa masoko.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake