Friday, May 24, 2024

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA RAIS WA CAF



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika(CAF) kwa kuifanya Zanzibar kuwa mmoja ya waandaaji wa Mashindano ya African Football Championship mwaka huu.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Dk.Patrice Motsepe na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 24 Mei 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar itaendeleza na kudumisha uhusiano wake na CAF.

Rais Dk.Mwinyi amemueleza Dk.Motsepe kuwa Zanzibar inahitaji msaada wa kuendeleza vipaji vya soka kuanzia ngazi za academy kwa kushirikiana na CAF.

Rais wa CAF Dk.Motsepe leo atashuhudia mchezo wa kwanza wa fainali za Mashindano ya African Schools Football Championship yanayofanyika katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Dkt.Patrice Motsepe akisaini mpira kwa ajili ya kumkabidhi zawadi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 24-5-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Jezi ya Timu ya Taifa ya Zanzibar Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Dkt.Patrice Motsepe, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika m azungumzo na ujumbe wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ukiongozwa na Rais wa Shirikisjho hilo, Dkt.Patrice Motsepe, Ikulu ya Zanzibar ei 24, 2024.






RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Dkt.Patrice Motsepe na ujumbe wake baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu

No comments: