RAIS wa Iran Ebrahim Raisi (63,) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kutoka Kaskazini Magharibi mwa Nchi hiyo kuanguka AFP Reuters imeripoti.
Ebrahim aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Hussein Amirabdollahian pamoja na viongozi wengine ambao wote wamepoteza maisha katika ajali hiyo wakitokea katika shughuli za kikazi mpakani mwa Iran na Azerbaijan.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mabadiliko ya hali ya hewa huku ikielezwa kuwa helikopita hiyo ilipata ajali karibu na eneo la Jolfa, zaidi ya kilomita 600 kutoka Tehran karibu na mpaka na Azerbaijan.
Licha ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kutuma usaidizi wa waokoaji 50 na ndege mbili za kusaidia zoezi la uokoaji taarifa zimeeleza kuwa mabaki ya helikopta yaliyopatikana yamedhiirisha hakuna aliyenusurika
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake