Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kujihusisha na mchezo mchafu wa kushikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi.
Bashungwa ameyasema hayo wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, Bungeni jijini Dodoma leo, Mei 29, 2024
Amesema changamoto kubwa ni uwepo wa vishoka wanaoshikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi na kutoza fedha nyingi.
Bashungwa amesema Wizara ya Ujenzi inaendelea na mazungumzo na Wizara ya Madini kuhusu upatikanaji wa malighafi ya ujenzi ikiwemo changarawe, mchanga na kokoto.
“Mazungumzo hayo yanalenga kupata namna bora ya kutatua changamoto kubwa ya upatikanaji wa malighafi hizo.” amesema Bashungwa
“Dhamira ya Wizara ni kuwa kwa kadri inavyowezekana maeneo hayo yamilikishwe TANROADS ili kuwezesha miradi mingi ya barabara kutekelezwa kwa wakati, na kupunguza gharama za ujenzi.”
Amesema Upatikanaji wa malighafi ya ujenzi kwa gharama nafuu itawezekana iwapo TANROADS itakuwa na maeneo ya kuchimba madini ya ujenzi na kuondokana na hali ya sasa ya vishoka wanaopandisha gharama za ujenzi.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake