Wednesday, July 24, 2024

KIJANA WA MIAKA 19 AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA UBAKAJI NA ULAWITI.


Na John Walter -Babati
Mahakama ya wilaya ya Babati mkoani Manyara imemtia hatiani Kijana Ramadhani Iddi Kipusa (19) kutumikia kufungo cha miaka 30 jela kwa makosa mawili ya kubaka na kumlawiti binti mlemavu (Bubu) mwenye umri wa miaka 19 nakutakiwa kulipa fidia Laki 5 kwa kila kosa.

Hukumu hiyo katika kesi ya jinai namba 5310/ 2024 jamhuri dhidi ya Ramadhani Iddi Kibusa, imesomwa mbele ya Mahakama na hakimu wa mahakama ya wilaya ya Babati Martin Masao.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na jamhuri dhidi Kijana huyo, mahakama imejiridhishwa pasina shaka kuwa Ramadhani Iddi Kipusa alimbaka na kumlawiti binti huyo.

Aidha hakimu Martin Masao amesema mtuhumiwa Ramadhani Iddi Kipusa (19) ametiwa hatiani Kwa makosa mawili ya kubaka na kulawiti ambapo Kwa kosa la kubaka mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume cha kifungu Cha sheria namba 130 (1) na kifungu kidogo Cha 2 (a) ikisomwa sambamba na kifungu 131(1) ambacho kinatoa adhabu, na kosa la pili la kulawiti kinyume cha kifungu cha sheria namba 154 (1)(a) Cha sheria ya kanuni za adhabu sura namba 6 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Kijana Ramadan Iddi Kipusa ametiwa hatiani kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 30 Kwa Kila kosa ambapo atatumikia kwa wakati mmoja na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi laki 5 Kwa Kila kosa.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali mkoa wa Manyara Chema Maswi amesema upande wa jamhuri wameridhishwa na hukumu hiyo na kwamba itakuwa fundisho Kwa watu wengine wenye tabia za kufanya matukio ya ukatili wa kijinsia.

No comments: