Tukio hilo limefanyika Agosti 06,2024 katika Kijiji cha Pantamela na Mji wa Mkwajuni wilayani humo kwa lengo la ulinzi wa mali na dhahabu katika maeneo hayo ili waweze kufanya biashara katika mazingira salama ambayo yataondoa viashiria vya uhalifu na wahalifu.
Aidha, Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linaendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa elimu na kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya uhalifu na ukatili wa kijinsia ili jamii iendelee kuchukia matendo yote maovu pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi hilo ili kuzuia, kukomesha vitendo hivyo katika jamii.
Sambamba na hilo Kamanda Senga alifanya ukaguzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda Mkoa wa Songwe linalojengwa eneo la Nselewa Wilaya ya Mbozi ambao ujenzi wake bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment