Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe . Haroun Ali Suleiman akitoa nasaha kwa watendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora juu ya namna ya kukusanya moni kwa wadau mara baada ya kuwasilishwa mpango kazi wa kitaifa wa haki za binaadamu na biashara katika ukumbi wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mazizini.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadam na Utawala Bora, Mohamed Khamis Hamad akiufahamisha mpango kazi wa kitaifa wa haki za binaadamu na biashara kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe . Haroun Ali Suleiman huko katika Ukumbi wa Wizara hiyo, Mazizini .
Na Khadija Khamis – Maelezo
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadam na Utawala Bora, Mohamed Khamis Hamad amesema zoezi la kukusanya maoni na taarifa muhimu kwa wadau litasaidia kupata namna bora ya kuandaa mpango kazi wa kitaifa wa haki za binaadamu na biashara nchini .
Akizungumza mara baada ya kikao cha kujadili hatua iliyofikia ya kukusanya maoni kwa wadau mbali mbali huko katika ukumbi wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mazizini .
Amesema kuwa zoezi hili tayari limekamilika kwa upande wa Unguja hivyo mapendekezo hayo yanaendelea kufanyiwa uchambuzi ili kuandaa mpango huo kwa ufanisi.
Aidha, amefahamisha kuwa wamepokea changamoto na mapendekezo katika zoezi hilo ambayo yatawasaidia kwa kuyafanyia kazi jambo ambalo ndio msingi wa kutengeneza mpango huo.
Amefahamisha kuwa baadh ya maoni ya wadau hao kubadilishwa kwa baadhi ya sheria ambazo zimepitwa na wakati pamoja na baadhi ya watendaji kukosa usimamizi mzuri wakati wa utoaji huduma licha ya kuwepo sera na sheria .
Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe . Haroun Ali Suleiman amewataka watendaji wa tume hiyo kuwaelekeza vizuri wananchi mambo ambayo wanayoyahitaji ili kufikia lengo walilolikusudia .
“Tuwe makini tusije kosea njia tukazungumzia mambo ya kisiasa baada ya kiuchumi na kibiashara hasa hasa tufike kwa wananchi wenyewe .”alisema Waziri Haroun.
Jumla ya maeneo saba ambayo ni vipaumbele vya kisekta ambayo yameidhinishwa na Kamati Tendaji ya Kitaifa kufanyiwa zoezi hilo katika maeneo ya kilimo na Uchumi wa Bluu, Utalii na Ukarimu, Kazi na Usafirishaji. Biashara na Fedha, Uzinduaji, Nishati, pamoja na Mawasiliano ya Kidigitali .
Zoezi la ukusanyaji maoni na taarifa muhimu limeanzia tarehe 29, Julai hadi tarehe 02 Agosti mwezi huu kwa upande wa Zanzibar .
No comments:
Post a Comment