ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 11, 2024

NCHIMBI AHITIMISHA KAGERA MKUTANO MKUBWA MULEBA



-Wapinzani wazidi kupukutika wakirejea CCM

Maelfu ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Wananchi wa Muleba wakiwa wamejitokeza na kukusanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, Muleba mjini, Mkoa wa Kagera, leo Jumapili 11 Agosti 2024, kwa ajili ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, wakati akihitimisha ziara yake ya siku 6, mkoani humo.
Balozi Nchimbi alianza ziara ya Mkoa wa Kagera Agosti 6, 2024 kwa kupokelewa eneo la Nyakanazi, Biharamulo akitokea Mkoa wa Kigoma.

Katika ziara hiyo yenye malengo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025 kuhamasisha uhai wa Chama na kusikiliza na kuzungumza na wananchi, Balozi Nchimbi ameongozana Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) - Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Abdalla Hamid, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Katika mkutano huo pia, viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, wakiongozwa na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Kata hiyo, walirudisha kadi zao za vyama hivyo na kurejea CCM, wakitambua kazi kubwa inayofanywa na Chama Cha Mapinduzi, pia Serikali zake, chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuiongoza nchi na Watanzania.

No comments: