Saturday, August 24, 2024

RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN MWINYI AMAMEITAKA JAMII KUWEKA MKAZI KWENYE MALEZI YA VIJANA NA WATOTO


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini alipowasili katika viwanja vya Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja, kuhudhuria Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 23-8-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa, iliyofanyika katika Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2024.
BAADHI ya Wajumbe wa Baraza la Maulamaa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia Waumini, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2024.
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia Waumini, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2024.
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2024, na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman Chum.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wananchi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2024.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dk, Hussein Ali Mwinyi ameinasihi jamii kuweka mkazo kwenye malezi ya vijana na watoto ili kuwanusuru na mmomonyoko wa maadili.

Alhaj Dk, Mwinyi ametoa tamko hilo leo tarehe 23 Agosti 2024 wakati akitoa salamu baada ya kujumuika pamoja na waumini wa Kiislam kwenye sala ya Ijumaa, Msikiti Shuraa uliopo Magomeni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Ameeleza kumekuwa na mmonyoko mkubwa wa maadili na vitendo viovu vinavyosababishwa na vijana wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe uliokithiri.

Amewahimiza wazazi kuhakikisha vijana wanapata elimu ya dini kwa ajili ya kujitambua na kujiepusha na vitendo viovu.

Alhaj Dk, Mwinyi amefahamisha Zanzibar ilikuwa nchi yenye sifa na kusimamia maadili lakini yameporomoka kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kwa kundi kubwa la vijana.

Aidha, amewahimiza viongozi wa dini kuendelea kuhubiri na kuwahimiza waumini kufuata misingi ya dini ili kuirejesha nchi katika maadili mema.

Mapema Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume amewashauri Watumiaji wa vileo kufikiria madhara ya mihadarati wanayotumia badala ya kufikiria starehe ya muda mfupi.

Sheikh Khalid amesema, dini ya kiislamu imekataza matumizi ya pombe kwa kufahamu athari zake kwa mtumiaji na jamii na kusisitiza kwa vijana kurudi katika misingi ya dini ili kujinusuru.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake