RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akibeba jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Hassan Omar (Mkele) mmoja wa Watanzania aliyebeba udongo wa Muungano Kati ya Zanzibar na Tanganyika, kabla ya kuaza kwa Sala ya Maiti iliyofanyika katika Msikiti wa Kibweni Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 28-8-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali,Wananchi na WA Vyama vya Siasa,katika Sala ya Maiti, kuusalia mwili wa marehemu Hassan Omar (Mkele) iliyofanyika katika Msikiti wa Kibweni Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, iliyongozwa na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Dkt. Maalim Siasa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Alhajj.Dkt. Mohammed Said Dimwa. (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo katika kaburi likiwa na mwili wa marehemu Hassan Omar (Mkele) mmoja wa Watanzania waliochanganya Udongo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wakati wa maziko hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Kibweni Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 28-8-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Hassan Omar (Mkele) mmoja wa Watanzania waliobeba udongo wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika, katika miaka ya Siti, ikisomwa na Maalim Dkt.Siasa, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika Makaburi ya Kibweni Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 28-8-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akzungumza na kutowa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu Hassan Omar (Mkele) mmoja wa Watanzania waliobeba udongo wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika, katika miaka ya Siti,alipofika nyumbani kwa marehemu Kibweni Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 28-8-2024, kutoa mkono wa pole kwa familia.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment