Na Leluu Majjid ,Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesifu ujasiri na uzalendo alionao Mwanasiasa Mkongwe Baraka Mohamed Shamte kwa kuweza kukwepa ghiliba na hadaa za upinzani na kuendelea kuiunga mkono CCM.
Pia chama hicho kimesema uamuzi wake wa kuzungumzia maendeleo yaliopatikana kwa muda mfupi Zanzibar ameonyesha uungwana na kujua ukweli.
Msimamo huo umetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi na Uenezi, Khamis Mbetto Khamis, aliyemtaja Mzee Shamte siku zote amekuwa mtu jasiri.
Mbetto alisema Mwasiasa huyo toka enzi za ASP baadae CCM,aliwahi kuteleza na kwenda kinyume na maadili ya Chama akavuliwa uanachama wake.
'Amethamini juhudu za serikali ya awamu ya nane kwa hatua zinazochukuliwa na SMZ chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi. Taratibu za kumrudishia rasmi uanachama wake zitaelekezwa"Alifafanua Mbetto
Aidha alimtaja Mwanasiasa huyo ni mdau mkubwa wa maendeleo hivyo kutokana na kuvutiwa kwake na ufanisi wa SMZ,amejitokeza kuonyesha hisia zake za kizalendo .
"Ameitumikia Zanzibar tokea enzi za ukoloni .Amekuwa Naibu Katibu Mkuu ASP Youth League .Ameshakuwa Katibu wa CCM Wilaya, Mwenezi wa Wilaya ya Mjini Unguja Kichama. Alipovuliwa uanachama wake hakubabaika. Amekuwa muungwana taratibu zitaelekezwa kumrudishia uanachama wake" Alisema Mbetto.
Aidha Katibu huyo Mwenezi alisema mzee huyo mara zote amekuwa akiitakia mema CCM,ndiyo maana hata alipofuatwa na baadhi ya vyama vya siasa wakimtaka ajiunge navyo , aliwakatalia .
"Ameona utendaji wa Serikili ya Dk Mwinyi inavyochapa kazi Amekubali ukweli kutokana na dhamira yake ya kujenga nchi na kutumikia wananchi na nchi" Alieleza
Alisema CCM kwa kujua historia yake na mchango wake kwa Zanzibar,hivyo maelekezo ya vikao vya kikatiba vitafanyika ili kutimiza matakwa na kutoa maazimio mengine.
"Awali hakutambua malengo na kusudio la Rais Dkt Mwinyi katika mtazamo wa muda mfupi na mrefu .Kujikwaa si kuanguka .Ameelewa ,amejisahihisha na sasa atashirikishwa kusukuma mbele jahazi la maendeleo "Alisema Mbetto.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake