Wednesday, October 2, 2024

ECOBANK TANZANIA YAWAKUTANISHA WATEJA WAKE JIJINI MWANZA


Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Charles Asiedu akizunguma na wateja wa Benki hiyo wa jijini Mwanza ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja pamoja na kutambulisha huduma zake mpya  za benki hiyo.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu akiwakaribisha na kutoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na Benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Mwanza.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Ecobank Tanzania, Joyce Ndyetabura akizungumza kuhusu akizungumza kuhusu programu mpya ya mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati  kwa wateja wa benki hiyo wakati wa wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Mwanza.
Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi, Ruth Mwaiselage akizungumza kuhusu akizungumzia kuhusu wateja walioko nje ya nchi zenye huduma za Ecobank watahudumiwa sawa na wale walipo hapa nchini wakati wa maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa Wateja jijini Mwanza.
Baadhi ya wateja wa Ecobank Tanzania wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na viongozi wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa Wateja jijini Mwanza.

Wakati dunia ikiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Ecobank Tanzania imeungana na ulimwengu mwezi huu wa Oktoba kuadhimisha wiki hiyo kwa kualika wateja wake wa jijini Mwanza pamoja na kutambulisha huduma zake mpya ambazo zitasaidia wateja wake.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Charles Asiedu amesema benki hiyo imejidhatiti kutoa suluhu kwa wateja wa huduma za kifedha kwa masharti nafuu pamoja na huduma ya kibenki kwa wateja wanaotumia huduma za benki hiyo nje ya nchi

Pia amesema hivi sasa wamekuja na programu ya mikopo yenye riba nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakipata changamoto hasa wanapotaka kuchukua mikopo hivyo Ecobank Tanzania imekuja na suluhu kwa wateja hao.

Bidhaa mpya iliyotambulishwa kwa wateja wa Benki hiyo itasaidia kutatua changamoto kwenye biashara hususani mipakani, utatuzi wa masuala ya fedha katika uchimbaji madini, uvuvi na usafirishaji na huduma za masuala ya benki binafsi.

Wiki ya huduma kwa wateja imekuwa ni fursa nzuri kuungana na wateja, kuwafahamu zaidi, kujibu maswali yao, kusikia kero zao, mapendekezo yao na nini kifanyike ili kuondoa changamoto zote.

No comments: