ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 2, 2024

PINDA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI DODOMA


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akiongoza kikao cha usuluhishi wa mgogoro wa ardhi kati ya bw. Emmanuel Cornel Mbunda na Familia ya Mzee Broma Michael Mtega katika ofisi yake iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akimkabidhi Bi.Mary Mtega Michael muhstasari wa makubaliano ya usuluhishi wa mgogoro wa ardhi kati ya Emmanuel Cornel Mbunda na Familia ya Mzee Broma Michael Mtega katika ofisi yake iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akishuhudia mapatano ya amani ya usuluhishi wa mgogoro wa ardhi kati ya bwn. Emmanuel Cornel Mbunda (kulia) na Familia ya Mzee Broma Michael Mtega (kushoto) katika ofisi yake iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu Dodoma
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amemaliza mgogoro wa Ardhi wa Familia ya Bw. Emmanuel Corneli Mbunda na Mzee Broma Michael Mtega.

Mhe. Pinda amemaliza mgogoro huo tarehe 31 Oktoba 2024 katika ofisi yake iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma, kwa kufanya kikao na pande zote mbili zenye mgogoro na kisha kufikia maridhiano.

Mgogoro huo unahusisha kiwanja Namba 109 na 110 vilivyopo katika Kitalu D eneo la Swaswa Ng'ambo Jijini Dodoma ambapo Msingi wa Mgogoro huo ni Bwn. Emmanuel Cornery Mbunda Mwenye Kiwanja 109 kujenga ukuta kwenye eneo la Bw. Broma Michael Mtega mwenye kiwanja Namba 110.

Mara baada ya kusikiliza pande zote kwa kuchambua nyaraka za wamiliki hao, Mhe Pinda alibaini kuwa Bw Emmanuel Mbunda aliuziwa eneo la mita za mraba 650, hata hivyo eno ambalo amelitumia kujenga ukuta lina ukubwa wa mita za mraba 986 ikiwa ni zaidi ya eneo lake kwa mujibu wa nyaraka ikiwemo ramani inayoonesha Kiwanja Na.109 kina Ukubwa wa mita za mraba 467 na kiwanja Na. 110 kina ukubwa wa mita za mraba 519.

Pande zote katika mgogoro huo zimeridhia kwa kauli moja kwa kusaini mbele ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ardhi kwa kufanya marekebisho ya mipaka kwa kuhusisha wataalamu wa ardhi ili kumaliza mgogoro huo ambapo Mhe. Pinda ameelekeza marekebisho hayo yafanyike Kuanzia tarehe 01/11/2024.

No comments: