Thursday, November 7, 2024

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WANAWAKE WAGOMBEA SERIKALI ZA MITAA


Afisa wa Program Mafunzo wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu dhana za jinsia na ushiriki wa Wanawake katika uongozi kwa washiriki kutoka vyama vya siasa mbalimbali katika warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakichangia mada kwenye warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, Chama cha Kijamii (CCK) na NCCR Mageuzi wakifuatilia ufunguzi pamoja na mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umeendelea na utaratibu wake wa kujengea uwezo wanawake viongozi katika Mamlaka za serikali za Mitaa ili waweze kuendeelea kubeba agenda ya usawa wa Kijinsia katika uongozi na kuwezesha wanawake wanaotarajiwa kuwa viongozi kujenga hoja zenye mtazamo wa kijinsia zitakazokubalika na wananchi

Mafunzo hayo ya siku mbili, yanawahusisha wanawake kutoka vyama mbalimbali vya siasa, kutoka manispaa za Dar es salaam, wilaya ya Kibaha na Chalinze mkoani Pwani na Morogoro, ambao wanajengewa uwezo juu ya umuhimu wa ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi, masuala muhimu ya kijinsia ya kufanyia kazi wakati wa kuandaa mipango ya bajeti, miongozo na ushiriki wa wanawake kwenye kamati za ardhi, shule, bodi za shule, kamati za zahanati na kamati za vituo vya afya.

Aidha, wamnejengewa uwezo juu ya ujenzi wa nguvu ya pamoja kama wanawake ili waweze kushikamana na kuwezesha wanawake wengi zaidi kushiriki kwenye nafasi mbalkimbali za uongozi ili kusimamia ajenda ya maendeleo shirikishi kwa wote.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake