RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, Uimariahaji wa Miundombinu katika Viwanja vya ndege kunalenga kuvifanya kuwa bora na kutoa huduma kulingana na vigezo vya Kimataifa.
Rais Dk. Mwinyi ametoa tamko hilo alipozindua miradi mitano ya Miundombinu mbalimbali katika kiwanja cha Kimataifa Cha Abeid Amani Karume, Wilaya ya Magharibi B, ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dk. Mwinyi ameeleza kuwa lengo ni kuwa na Viwanja vya ndege vyenye sifa ya utoaji wa huduma bora kwa abiria zitazokidhi mahitaji ya ongezeko la wageni wanaoingia nchini kila siku.
Amefahamisha kuwa miradi mitano alioizindua itaufanya Uwanja huo kuwa wa kujivunia na hadhi ya Kimataifa katika Afrika na duniani kwa utoaji wa huduma bora zitakazoridhiwa na wageni.
Miradi aliyoizindua Dk. Mwinyi ni pamoja Uwekaji wa mawe ya msingi kwa majengo ya abiria “Termninal One na Two, ambayo ameielezea itajumuisha ujenzi wa jengo la viongozi na wageni mashuhuri (VIP) utakaotumiwa pia na wafanyabiashara wakubwa, kupokea ndege binafsi za wageni mashuri.
Akizungumzia ujenzi wa kituo cha kisasa cha biashara Rais Dk. Mwinyi ameleza ujenzi huo utahusishwa majengo ya benki, mikahawa mikubwa ya kimataifa na maofisi yatakayotoa huduma saa 24 kwa wageni na watumiaji wa uwanja huo pamoja na uzinduzi wa taa mpya za kuongozea Ndege na mradi wa kituo cha mafuta ya ndege ambacho Dk. Mwinyi amekielezea kuwa kitaleta ushindani kwa utoaji wa huduma za mafuta kwa ndege zinazotua uwanjani hapo na kutoa unafuu wa bei na kupunguza safari za ndege kwenda kuweka mafuta nje ya Zanzibar.
Akizungumzia Uwanja wa ndege wa Pemba amesema Serikali imekusudia kuujenga uwanja huo kuwa wa kimataifa kwa kuutanua na kuongeza njia za kuruka na kutua ndege “Run way” ili kuifungua Pemba kibiashara.
Aidha, amesema Pemba ijayo itapokea wageni na watalii moja kwa maja badala ya kushuka Zanzibar na hatimaye kuunganisha ndege nyengine Kwenda Pemba. Sambamba na ujenzi wa bandari za Mkoani, Wete na Shumba Mjini ili kuikuza Pemba kwa utalii, biashara na uwekezaji.
Vilevile, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuridhishwa kwake na kazi kubwa inayofanywa na Mamkala ya Viwanja vya ndege (ZAA) hususan mabadiliko ya utendaji yanayozingatia uwajibikaji na nidhamu pia kusifu juhudi kubwa wanayoifanya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuufanya uwanja huo kupokea wageni wengi zaidi.
Akizungumzia ukuaji wa utalii nchini amesema takriban watalii milioni mbili wanaingia nchini kila mwaka, hivyo kuna kila sababu kwa Serikali kuchukua juhudi maalum za kuimarisha viwanja vya ndege kwa miundombinu bora.
Rais Dk. Mwinyi ameahidi ujenzi wa hoteli kubwa zenye hadhi ya juu ili kuwavutia wageni wengi zaidi hatua itakaimarisha utalii na kuongeza mapato yanatotokana na sekta huyo muhimu kiuchumi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Khalid Salum Mohamed amemshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa busara na miongozo anayoitoa kwa Wizara hiyo ambayo imechangia maendeleo makubwa ya viwanja vya ndege nchini na kumpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari
Pamoja na kusifia kazi kubwa inayofanywa na mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar hadi kupata tunzo za kimataifa kufuatia mabadiliko ya utendaji katika mamlaka hiyo ya utowaji wa huduma bora.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege vya Zanzibar ZAA, Seif Abdalla Juma amsema ujenzi wa majengo ya Abiria ya “Terminal One na Two” na kituo cha kisasa cha biashara yanagharamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa fedha zake wenyewe ambapo ujenzi umefikia hatua nzuri na kuongeza kuwa ujenzi huo umetokana na kuchakaa kwa majengo ya zamani ambayo hayaendani na mahitaji ya sasa ya mabadikilo ya viwanja vya ndege dunuiani.
Amesema mbali ya mabadiliko makubwa kiwanjani hapo amesema, wanakusudia kuweka mfumo wa kisasa wa kuhifadhia makontena ya mizigo kwa lengo la kuendana na mahitaji na ubora wa viwanja vya sasa vya ndege duniani.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment