Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kumulia hali Muazilishi wa Madrasatul Maryam Mfenesini Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja,Bi.Maryam Omar Muhammed, kabla ya kuaza kwa Dua maalumu ya kumuombea , iliyofanyika leo 29-12-2024.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Viongozi na Waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea nchi amani wakati huu ikielekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Rais Alhaj Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipotoa salamu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Madrassa Maryam ya Mfenesini Wilaya ya Kaskazini B alipojumuika katika Dua Maalum ya Kumuombea ilioandaliwa na Madrassa.
Ameeleza kuwa mambo yote ya Maendeleo yataweza kufanyika ikiwa nchi itabaki na Amani na Wananchi kuwa na Umoja na Utulivu wa nchi.
Amefahamisha kuwa hakuna nchi yenye machafuko iliyopata Maendeleo hivyo kila mmoja ana wajibu wa kusisitiza Amani kwa maslahi ya nchi.
Alhaj Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Uzoefu unaonesha kuwa kwa muda mrefu nchi ilikuwa ikipata matatizo hususan wakati wa Uchaguzi hivyo ni vema mambo hayo yasijirudie tena kwa kuhubiri Amani ndani ya Jamii.
Kabla ya Dua hiyo maalum Alhaj Dk. Mwinyi alimjulia hali Mwanzilishi wa Madrassa hiyo Bi.Maryam Omar Muhammed.
No comments:
Post a Comment