Spika wa Baraza la Wawakilishi Zuberi Ali Maulid(kulia)akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi Ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Kulala Wageni (Moyo mzuri Villa Resort)Fukuchani Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,ambapo kauli mbiu "Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani,Umoja na Mshikamano kwa maendeleo yetu.
Na Ali Issa Maelezo
Spika wa Baraza la Wakilishi Zubeir Ali Maulid amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuvutia waekezaji katika sekta mbalimbali za kimaendeleo.
Ameyasema hayo huko fukuchani Mkoa wa kaskazini Unguja wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Biashara za kulala wageni zinazo milikiwa na kampuni ya Moyo mzuri villa Resot kufuatia shamra shamara za kuadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema nijambo la kujivunia kwa kuipa heshima Nchi kwa kuja wageni wengi waaina mbalimbali kuja kutalii na kupumzika jambo ambalo lina paswa kupongezwa.
“Kwa Mwaka wa 2023 Sekta ya utalii inaonesha kuwa idadi ya watalii wanao ingia nchini imezidi kuongezeka na kufikia walii zaidi ya laki sita na inalenga kufikia wageni milioni ifikapo 2030”alisema Spika wa Baraza la wakilishi.
Alisema kuwa kufanikiwa huko kunatokana na Serikali kuweka mazingira mazuri ya kisera na sheria ambayo imeweza kupanua wigo kwa kuibuka miradi mingi ya ujenzi wa nyumba za biashara.
Hatahivyo amezitaka tasisi zote zinazo husika ikiwemo ZIPA kufanya tathimini ya uekezaji wa nyumba za biashara kwa wageni na kuishauri serikali juu ya muelekeo sahihi wa kuimarisha utalii kwa maslahi ya nchi.
Nae Muekezaji Mzawa wa Mradi huo akitoa taarifa ya uwekezaji huo John Goason Mbwambo alimshukuru Rais Dr.Mwinyi kwa kuwaruhusu waekezaji kuwekeza hapa Zanzibar jambo ambalo lime mpa moyo kwa kumsaidia kupata frusa ya kuekeza mradi huo pamoja na kuwezeshwa kufikia hatua hiyo.
Aidha alisema kuwa mradi huo unathamani ya Dolla milioni moja 1 walizo azia lakini kwa sasa wameshatumia dola zaidi ya laki 4.
Nae mkurugenzi mtendaji kutoka Mamlaka kukuza vitega Uchumu Zanzibar ZIPA Saleh Said Muhamed alisema kuwa sekta ya uwezeshaji imesajili miradi zaidi 424 yenyethamani ya dola Bilioni 5.9 na kutegeneza ajira zaidi ya elfu 22 ni sawa na asilimia ambapo kwa mkoa huo wamesajili miradi 99 yenye thamani ya zaidi dola bilioni 2 za kimarekani.
Mapema mkuu wa Mkoa Kaskazini A Matar Zahoro Masuod alisema wananchi wa mkowa huo hawanabudi kuwaunga mkono viongozi wazalendo wa nchi hii kwa dhamira njema ya kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa huo.
No comments:
Post a Comment