ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 11, 2024

WAZIRI TABIA AMEFANYA ZIARA KUTEMBELEA CHUO CHA MCT AMANI


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akisikiliza maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Wanafunzi katika Chuo cha Mwenge Community Centre (MCT) Omar Abdalla Juma wakati Waziri huyo alifofanya ziara huko Amani, Wilaya ya Mjini.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akisikiliza maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Wanafunzi katika Chuo cha Mwenge Community Centre (MCT) Omar Abdalla Juma wakati Waziri huyo alifofanya ziara huko Amani, Wilaya ya Mjini.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akitoa ufafanuzi wa changamoto huko katika Chuo cha Mwenge Community Centre (MCT) kilichopo Amani, Wilaya ya Mjini.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Hiji Dadi Shajak katika Chuo cha Mwenge Community Centre (MCT) Amani, Wilaya ya Mjini.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo cha Mwenge Community Centre (MCT) huko Amani, Wilaya ya Mjini.

Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na UhusianoWHVUM.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita ameahidi kutoa Kompyuta 25, Air Condition 2 kwa Uongozi wa chuo cha Mwenge Community Centre (MCT) ili kutatua Changamoto zilizopo.

Mhe. Tabia ametoa Maagizo hayo hapo jana wakati alipofanya ziara katika Chuo hicho kilichopo Amani, Wilaya ya Mjini.

Amesema lengo la kuahidi vifaa hivyo ni kuunga mkono Chuo hicho na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla.

Aidha amesema vifaa hivyo vitasaidia kutoa taaluma kwa ufanisi ili kufikia malengo yaliokusudiwa ya kuwaandaa Vijana kuwa bora.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Hiji Dadi Shajak ameushauri Uongozi wa Chuo hicho kuwaandaa vijana wao na kuweza kufanya kazi zaidi ya moja ili kuleta ufanisi katika kazi.

‘‘Kwa wakati huu tulionao wa Sayansi na Teknolojia, lazima vijana Wafanya kazi zaidi ya moja kama vile kuediti, kuandika habari, kupiga picha, hii itarahisisha na kuleta Ufanisi katika Kazi’’ alisema Katibu Shajak.

Mapema akitoa maelezo katika ziara hiyo, Kiongozi wa Wanafunzi katika chuo hicho Omar Abdalla Juma amesema ziara hiyo imeleta faraja kwani wamepata fursa ya kuelezea changamoto zianazowakali ikiwemo uhaba wa eneo na vitendea kazi.

Ziara hiyo ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita imefanyika katika Kituo cha Bomba Fm, Mwenge Fm na kumjuilia hali Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Sleiman Ame Khamis huko Nyumbani kwake Sebleni Wilaya ya Mjini.

No comments: